Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk.Yahaya Nawanda
Mwenge wa uhuru Shinyanga kuifikia miradi 41 yenye thamani ya Sh.bilioni 14.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Ambapo mwenge huo ukiwa mkoani Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 na kuifikia miradi 41 yenye thamani ya Sh.bilioni 41.02.
"Katika Miradi hii, Miradi 11 itawekewa Mawe ya Msingi, 14 itazunduliwa, Minne itafunguliwa, na Miradi 12 itaonwa,"amesema Mndeme.
"Miradi hii imegharamiwa na Serikali kuu Sh.bilioni 8.7 Halmashauri Sh.bilioni 3.9, nguvu za wananchi Sh.milioni 116.4, Sekta binafsi na wahisani mbalimbali Sh.bilioni1.2," ameongeza.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kuupokea Mwenge huo ambao utakuwa ukipita katika maeneo yao na kwenye miradi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kwa ajili ya kuanza kukimbizwa wilayani humo.
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga zinaanza kukimbizwa katika wilaya ya Kishapu kwa kuzindua,kuweka mawe ya msingi na kuona jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Sh.bilioni
1.3.
Mbunge wa Solwa Ahmed Salum akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiushika Mwenge wa Uhuru.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464