BENKI YA CRDB YATOA ZAWADI KWA WATOTO WENYE UALBINO, YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO AMBAZO ZINAWAKABILI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
BENKI ya CRDB imetembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji Cha Buhangija Manispaa, na kuwafariji watoto wenye Ualbino huku wakiwasihi kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao, pamoja na kuwapatia zawadi ya vitu mbalimbali.
Watoto wenye Ualbino.
Akizungumza leo Julai 25, 2023 kwenye kituo hicho Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Timothy Fasha, amesema kupitia idara ya rasilimali hua wanakitengo cha kusaidia watu wenye uhitaji kwa kurudisha fadhira, ndipo wakawasiliana Shirika la Under the Same sun na kubainishiwa changamoto za kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Timothy Fasha.
Amesema Benki hiyo ipo pamoja na watoto hao wenye uhitaji, na watakuwa nao bega kwa bega katika safari yao ya elimu, na kuwasihi wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao, ili siku moja waje kuwa viongozi katika Taifa hili na hata Ma-Meneja wa Benki hiyo ya CRDB.
Watoto wenye Ualbino.
“Benki ya CRDB tuna furahi kujumuika na nyie watoto tunawasihi msome kwa bidii, na tunafarijika mnapofanya vizuri katika msomo yenu, na sisi tutaendelea kuwa na nyie bega kwa bega katika safari yenu ya elimu na kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili,”amesema Fasha.
Aidha, ametaja baadhi zawadi ambazo wamezitoa kuwa ni Juice, Biskuti, T-Sheti pamoja na Kofia kwa ajili ya kuwalinda na Jua.
Maafisa wa Benki ya CRDB wakigawa Kofia kwa watoto wenye Ualbino.
Naye Mgeni Rasmi Afisa Elimu Msingi na Awali Manispaa ya Shinyanga Mary Maka, ameipongeza Benki hiyo kwa kujitoa kusaidia watoto hao wenye uhitaji, na kubainisha kuwa kazi ambayo wameifanya ni jambo la kimungu.
Afisa Elimu Msingi na Awali Manispaa ya Shinyanga Mary Maka.
“Kandri mnavyotoa ndipo mnavyozidi kupokea tunawashukuru Benki ya CRDB kwa kushiriki Baraka hizi, tunatoa wito kwa watu wengine zikiwamo Taasisi mbalimbali waendelea kusaidia watu wenye uhitaji,”amesema Maka.
Nao watoto wenye Ualbino akiwamo John Daima, ameishukuru CRDB kwa kuwatembelea na kuwapatia nasaha za kusoma kwa bidii, pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali.
John Daima.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi ambaye ndiye mlezi wa kituo hicho Fatuma Jilala, amesema kuna Jumla ya watoto wenye Ualbino 78, na kushukuru wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza na kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo bado zinawakabili kituoni hapo.
Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi ambaye ndiye mlezi wa kituo hicho Fatuma Jilala.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Timothy Fasha, akizungumza na watoto wenye Ualbino.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney akizungumza na watoto wenye Ualbino.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana wakizungumza na watoto wenye Ualbino.
Meneja Afya ya Wafanyakazi kazini kutoka CRDB Makao Makuu Crescensia Kajiru akizungunza na watoto wenye Ualbino.
Meneja Rasilimali watu CRDB Kanda ya Magharibi Benjamini Ngayiwa akizungunza na watoto wenye Ualbino.
Viongozi na Maofisa kutoka Benki ya CRDB wakiwa meza kuu.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wafanyakazi kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Timothy Fasha,(kulia) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddy akigawa T-Shet zenye Nembo ya CRDB kwa watoto wenye Ualbino.
Ugawaji wa T-Shet ukiendelea.
Ugawaji wa Kofia ukiendelea.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Jummane Wagana akimvalisha Kofi Mtoto mwenye Ualbino yenye Nembo ya CRDB.
Watoto wenye Ualbino wakikabidhiwa zawadi ya Juice.
Muonekano wa zawadi.
Picha za pamoja zikipigwa na watoto wenye Ualbino.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464