Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude amefanya ziara katika mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi Mwadui (Williamson Diamond LTD), uliopo wilayani Kishapu ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa bwawa la maji tope.
Amefanya ziara hiyo leo Julai 10, 2023 akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko aliyoyatoa Juni 30 mwaka huu akitaka mgodi huo kufunguliwa rasmi Julai 15, 2023.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Mkude amesema kwa hatua iliyofikiwa ya utengenezaji wa bwawa hilo pamoja na miundombinu mingine anatumaini kuona mgodi huo unaanza rasmi uzalishaji na kupeleka manufaa kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464