Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh. Johari Samizi akikagua Ujenzi wa mojawapo ya Madarasa yanayotekelezwa kupitia fedha za BOOST katika Shule ya Msingi Manheigana kata ya Solwa-Halmashauri ya Shinyanga.
Na Mwandishi wetu-Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi Johari Samizi amesema kuwa ifikapo July 19 mwaka huu miradi yote ya ujenzi wa Madarasa katika shule saba (7) za Msingi halmashauri ya Shinyanga zinazotekelezwa kupitia fedha za Boost yatakuwa yamekamilika.Moja ya jengo la darasa katika Shule ya msingi Solwa yanayojengwa kupitia mradi wa BOOST.
Amebainisha hayo mapema leo July 12, alipotembelea ,na kukagua hali ya ujenzi huo na hatua iliyofikia ambapo amesema lengo la Serikali ni kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa watoto wa shule za Msingi ili waweze kuendelea kufanya vizuri zaidi katika Masomo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimuangalia mwanafunzi wa Shule ya Msingi Solwa.
Aidha Samizi amewataka wasimamizi wa miradi yote inayotekelezwa katika Wilaya hiyo kujenga utamaduni wa kuwashirikisha wananchi ili waweze kuona thamani ya miradi hiyo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akisikiliza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Solwa Hawadh Mbarouk wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya BOOST.
Samizi amesema jamii ikishirikishwa katika kazi mbalimbali ikiwemo shughuli za ujenzi, uchimbaji msingi,usombaji wa matofali, maji itasaidia kupunguza gharama katika ujenzi huo.Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya amewataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanafuatilia na kutoa maelekezo ya karibu pale inapotokea changamoto katika uteelezaji wake ili kuondoa kutumia gharama kubwa katika ujenzi huo.Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa madarasa katika shule hizo za Msingi zilizotembelewa na kukaguliwa hatua za ujenzi zilipofikia
Samizi amemtaka Mhandisi wa halmashauri ya William John Lusiu kuhakikisha ujenzi wote unafuata BOQ zilizoanishwa katika mkataba uliotolewa.
Mh.Samizi amewataka mafundi wanaotekeleza ujenzi wa madarasa hayo kuongeza kasi na kukamilisha haraka madarasa hayo. Ukaguzi ukiendelea
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Berege amesema kuwa moja ya changamoto iliyochangi kuchelewa kukamilika kwa wakati madarasa hayo ni ucheleweshaji wa materio yaliyokuwa yakitumika ikiwemo Saruji na Mabati hali iliyochangia kupungua kwa kasi ya ujenzi kwa baadhi ya shule.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Simon Berege akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi katika Ukaguzi wa Miradi ya BOOST
Berege amesema kuwa kwa sasa kasi ya ujenzi inaridhisha kutokana na uwepo wa matirio yote tendanishi ambapo madarasa yote yamefikia asilimia zaidi ya 90 ya utekelezaji wake. Ukaguzi ukiendelea
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga amewashauri watendaji wa halmashauri ya Shinyanga kuzingatia gharama za ujenzi kadri zilivyoanishwa kwenye maelekezo ya Serikali juu ya ujenzi huo.Kitinga amewataka wasimamizi wa ujenzi wa miradi mbalimbali kuwa na mawasiliano ya karibu miongoni mwao ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza ikiwemo kujengwa chini ya kiwango, kutofuata maelekezo ya ujenzi pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.Madarasa yakiendelea kukamilishwa katika Shule y msingi Bubale.
Katibu tawala huyo wa wilaya amewashauri watendaji na wasimamizi wa miradi kabla ya kuanza mradi wowote viongozi wa maeneo husika na halmashauri kuketi meza moja ili kuweka mpango mkakati wa pamoja katika ujenzi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.Nao baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi zinazotekeleza Mradi wa Madarasa kupitia fedha za BOOST akiwemo Said Jamaly, Dotto Shija wamesema ujenzi wa miundombinu hiyo ya madarasa utasaidia kuimairisha na kuboresha kiwango cha taaluma shuleni na hamasa kwa watoto katika kuhudhuria masomo kwa kuwa miundombinu hiyo imejengwa kwa ubora na mazingira ya sasa.Ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi imeambatana na Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara halmashauri hiyo, Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya,watalaamu mbalimbali, Katibu tawala wa Wilaya.Shule zilizotembelewa kukaguliwa ni Shule za Msingi Manheigana, Solwa, Mhangu A, Songambele, Bubale, Kashishi,Mhangu B, na Shule ya Msini Mwakitlyo.
TAZAMA PICHA MBALIMBALI.