WAKILI MADELEKA AFUTIWA KESI YA 'PLEA BARGAINING 'AKAMATWA TENA


Wakili Madeleka afutiwa kesi ya ‘plea bargaining’, akamatwa tena
Wakili Peter Madeleka (kulia) akiwa anajadiliana na Wakili wake, Simon Mbwambo (kushoto) katika kumbi ya Mahakama Kuu Arusha, muda mfupi kabla ya kukamatwa na polisi. Picha Mussa Juma.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemkamata Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka mara baada ya kufutiwa kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa.


Arusha. Wakili wa kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Madeleka kabla ya kukamatwa alilazimika kung'ang'ania kwa zaidi ya dakika 30 katika chumba cha Mahakama cha Jaji Aisha Bade ambaye awali ndiye alitoa maamuzi katika kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa ‘Plea bargaining.’

Wakili Madeleka aliwasilisha maombi namba 80 ya mwaka 2021 kutokana na kesi aliyokuwa amefunguliwa ya uhujumu uchumi namba 40/2020.

Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464