RC MNDEME AWAKARIBISHA WANANCHI WA SHINYANGA KUJITOKEZA KWA WINGI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU

RC MNDEME AWAKARIBISHA WANANCHI WA SHINYANGA KUJITOKEZA KWA WINGI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ana wakaribisha wananchi wote wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.

Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga utapokelewa kesho ukitokea mkoani Simiyu na utapokelewa wilayani Kishapu katika Shule ya Msingi Buganika.

Mndeme amebainisha hayo leo Julai 26, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilimota 571.5 na kuifikia Miradi 41 yenye thamani ya Sh.bilioni 41.02, na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuupokea, ikiwamo sehemu za miradi na kwenye Mkesha.

"Katika Miradi hii 41, Miradi 11 itawekewa Mawe ya Msingi, 14 itazunduliwa, Minne itafunguliwa, na Miradi 12 itaonwa,"amesema Mndeme.

"Miradi hii imegharamiwa na Serikali kuu Sh.bilioni 8.7 Halmashauri Sh.bilioni 3.9, nguvu za wananchi Sh.milioni 116.4, Sekta binafsi na wahisani mbalimbali Sh.bilioni1.2," ameongeza.

Hii hapa Ratiba ya Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga👇👇



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464