TAJOGEV WATOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAANDISHI WA HABARI MIKOA TISA

TAJOGEV watoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanadishi wa habari mikoa tisa.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MTANDAO wa Waandishi wa Habari wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Tanzania(TAJOGEV)umetoa elimu ya kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja waandishi wa habari kutoka mikoa tisa hapa nchini, katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Mafunzo hayo yametolewa leo Julai 13, 2023 Mkoani Shinyanga na yatahitimishwa kesho, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.

Mwenyekiti wa Mtandao wa waandishi wa habari za kupambana na ukatili Tanzania (TAJOGEV) Stella Ibengwe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, amesema lengo la kuanzisha Mtandao huo, ni kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, na mpaka sasa Mtandao umeshafikisha wanachama 96 kutoka mikoa 10.
Mwenyekiti wa (TAJOGEV) Stella Ibengwe.

Amesema wamewaita waandishi wa habari kutoka mikoa tisa, ambayo ni Mwanza, Mara, Kagera, Kigoma, Geita, Singida, Tabora, Simiyu na wenyeji Shinyanga, kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja katika masuala ya ukatili wa kijinsia kwa kuongeza nguvu ya pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

“Mtandao huu ni muhimu kwa Serikali katika mpango kazi wa Taifa (MTAKUWWA)wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto Tanzania kwa kutumia vyombo vya habari kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili,”amesema Ibengwe.

“Mtandao huu unaomba ushirikiano zaidi kwa Mamlaka za Serikali na watendaji wake ili kuwezesha kutokomeza ukatili wa kijinsia hapa nchi,”ameongeza.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Aidha, ametoa shukrani kwa mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga na SHYEVAWC kwa ushauri wao katika kuona Mtandao huo unafika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili.

Naye Mgeni Rasmi akifungua mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Waandishi wa habari katika Mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na kuahidi itashirikiana vyema na Mtandao huo ili kumaliza ukatili ndani ya jamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.

“Waziri wa Gwajima anafarijika kuona hayupo peke yake katika mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia, na kupitia Mtandao huu nawaomba muwafikie watu wote wakiwamo wanaume wapaze sauti za ukatili,”amesema Samizi.

Amewataka pia waandishi wa habari kupitia Mtandano huo wakaandike habari za kufichua mambo ya ukatili ambayo yamekuwa yakifichika ili yatatuliwe na kuisaidia jamii.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Nao baadhi ya waandishi wa habari, wamesema mafunzo hayo yamewaongezea ufanisi mkubwa wa kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa katika kuandika habari za kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji Deogratius Temba akitoa mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wakiwasilisha kazi za vikundi.
Kazi za vikundi zikiendelea kuwasilishwa.
Kazi za vikundi zikiendelea kuwasilishwa.
Kazi za vikundi zikiendelea kuwasilishwa.
Kazi za vikundi zikiendelea kuwasilishwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464