Wajumbe wa baraza la wanawake UWT Shinyanga mjini wakicheza baada ya kumkaribishwa mbunge viti maalumu Christina Mzava
Suzy Luhende, Shinyanga press blog
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewataka wajumbe wa baraza la Jumuiya hiyo kupendana, na kushirikiana kwa pamoja katika kufanya kazi mbalimbali za jumuiya na za chama ili kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo mwaka 2025, ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama wapya.
Hayo ameyasema leo Julai 8,2023 kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini lililofanyika katika ukumbi wa CCM Shinyanga mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa UWT mkoa akiwemo katibu Asha Kitandala na mwenyekiti Agnes Samweli.
Nhamanilo amesema viongozi wa Umoja wa wanawake CCM wakipendana na kushilikiana kwa pamoja na kuacha tofauti zote walizotoka nazo kwenye uchaguzi watafanya mambo makubwa ya kuifanya jumuiya kuwa na nguvu na kuweza kukijenga chama kuwa imara.
"Niwaombe viongozi wangu wote tupendane na tuwapende viongozi wetu tuliowachagua ambao wapo madarakani, tusibague kiongozi yeyote tushirikiane nao kwa pamoja ,pia tuwaombe wabunge wetu wasiwagawe wajumbe waonyeshe upendo kwa wote wasisikilize maneno ya wapambe yanayosababisha uchonganishi, waheshimiwa wawakatae,"amesema Nhamanilo.
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Sharifa Hassan Mdee amewataka viongozi wote wa kata kwenda kuhamasisha wanachama wa umoja huo wakalipie ada na wakajisajiri kwa mfumo wa Tehama,na kuhakikisha wanajisajili wengi katika umoja wetu na chama kwa ujumla.
"Pia niwaombe tukawe mabalozi kwa watoto wetu wa kike na wanawake tukiona mtoto anaozeshwa tutoe taarifa haraka katika mamlaka husika, kwani lengo letu ni kumkomboa mama na kuisaidia jumuiya yetu, nendeni mkawe mabalozi mkasimamie vizuri kuwakomboa watoto wa kike wasifanyiwe ukatili wa kuozeshwa wakiwa na umri mdogo wasiachishwe masomo, na tukahamasishe kina mama wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi," amesema Mdee.
"Pia nawashukuru sana wanawake kwa kunipokea vizuri nawaahidi kuwalipa kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa kutosha, na mimi nitakuwa kiunganishi kwa wanawake wote wa Shinyanga mjini, endapo kitatokea chochote tutaitana na kuzungumza kwa vikao sitaruhusu majungu yatawale kwenye jumuiya yetu, nitaruhusu upendo utawale,"amesema Katibu Mdee.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Christina Mzava amewaomba wanawake wote kuwa kitu kimoja kushirikiana kwa pamoja pale watakapokuwa na shughuli za jumuiya wawashirikishe wabunge wote watawasaidia pale watakapopungukiwa ili kuhakikisha kazi za jumuiya na chama zinaendelea.
"Huu ni wakati sasa wa kufanya kazi, hivyo tunatakiwa tuache tofauti zetu tufanye kazi mpaka tumalize muda wetu tunaomba mtufanye kuwa kitu kimoja ili tuweze kufanya kazi kwa ushirikiano, tuwe na umoja ambao ndio ushindi wetu, lengo ni kuenda vizuri ili kuhakikisha 2025 ushindi unapatikana,"amesema Mzava.
Naye katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Ally Majeshi amewataka wanawake waepuke kugawanywa gawanywa waendelee kuwa na umoja na wahakikishe wanafanya vikao kuanzia kwenye matawi, na wabunge wanapofika katika maeneo yao wapokee kero zilizopo na kuzitatua kwa wakati.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga amewataka wanawake wote kudumisha upendo na kufanya kazi kwa bidii bila kusahau kufundisha maadili mema kwa watoto ikiwa ni pamoja na kutenga muda wa kuzungumza na watoto ili wasijiingize kwenye maadili yasiyofaa.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga amesema wahakikishe wanasajili na kulipa ada kwa wakati ili kuhakikisha uhai wa jumuiya na chama unakuwepo, pia washirikiane vizuri na wabunge wao wote wasiwabague kwamba huyu ni wa furani na huyu ni wa furani ushirikiano utawale
Mwenyekiti wa UWT Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akiwa na katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Ally Majeshi wakiingia ukumbini kwenye kikao cha baraza la UWT
Mwenyekiti wa UWT Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee akizungumza na wajumbe wa baraza
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini
Sharifa Hassan Mdee
akizungumza na wajumbe wa baraza la Shinyanga mjini
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini
Sharifa Hassan Mdee
akizungumza na wajumbe wa baraza la Shinyanga mjini
Katibu wa IWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akizungumza kwenye baraza hilo
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza na wajumbe wa baraza hilo
Mbunge viti maalumu mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akizungumza na wajumbe wa baraza hilo
Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akizungumza kwenye baraza hilo
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee akizungumza na wajumbe wa baraza la Shinyanga mjini
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee akizungumza na wajumbe wa baraza la Shinyanga mjini
Mbunge viti maalumu mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akimpa fedha Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee
ya kuchukua kadi za wanachama wapya
Wajumbe wa baraza la UWT Shinyanga mjini wakiwa na zawadi ya kitenge wakienda kumzawadia katibu mpya wa UWT Shinyanga mjini Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga akiwa anasubiri zawadi yake kwa wanawake wa UWT Shinyanga mjini Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Hassan Mdee
Wajumbe wakamati ya utekelezaji UWT Shinyanga mjini na wajumbe wa baraza wakimsikiliza mwenyekiti akizungumza