Mwenge wa uhuru wazindua gari la wagongwa lililotolewa na wachimbaji wadogo wa dhahabu Mwakitolyo namba 5
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENGE wa Uhuru umezindua gari la wagonjwa ambalo limetolewa na wachimbaji Wadogo Mwakitolyo Namba 5, kwa ajili ya Zahanati ya Mwakitolyo na wilayani Shinyanga.
Mwenge umezindua gari hilo leo Julai 29,2023 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim katika Kituo cha Afya Tinde.
Muonekano wa gari la wagonjwa.
Akitoa taarifa ya gari hilo Mganga wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (DMO) Dk. Nuru Yunge amesema wachimbaji hao wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 walilinunua kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za usafiri katika Zahanati ya Mwakitolyo.
Muonekano wa gari la wagonjwa.
Amesema limekuwa na msaada mkubwa katika kuokoa vifo vya watu wakiwamo wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakijeruhiwa katika shughuli zao za uchimbaji kwa kuwahishwa Hospitali na kupata matibabu haraka.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amesema gari hilo la wagonjwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Mwakitolyo na hata vijiji vya jirani ambapo limekuwa likitoa huduma ya kuwahisha wagonjwa kupata matibabu na hata kuwakimbiza katika Hospitali za Rufaa na kuokoa Afya zao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, amewapongeza wachimbaji hao kwa kuunga Mkono Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
Baadhi ya viongozi wa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wilayani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja.
Picha ya pamoja ikipigwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha zikiendelea kupigwa kwenye gari la wagonjwa.
Meneja wa Vitalu katika Machimbo ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 Leonard Waziri akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kumulika Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa kuiona, kuikagua, kuweka Mawe ya Msingi pamoja na Mingine kuizindua.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464