Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana UVCCM wilaya ya Kishapu.
Na Marco Maduhu,KISHAPU
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Kishapu, imeendesha Mkutano wa Baraza la Vijana kwa kujadili ajenda mbalimbali za kuijenga Jumuiya hiyo, huku Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akiwataka vijana wasitumike vibaya kisiasa.
Mkutano huo wa Baraza la vijana (UVCCM) wilayani Kishapu umefanyika leo Julai 5,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu Benard Benson Werema.
Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu Benard Benson Werema, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, amesema wamefanya Mkutano wa Baraza la vijana ili kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya kuijenga Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu Benard Benson Werema.
Amesema Jumuiya ya vijana (UVCCM) ndiyo Jeshi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kuhakikisha Chama kinasimama imara pamoja na kupigania viongozi wa Chama hicho, na kusemea mambo mazuri ikiwamo miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kwa wananchi chini ya Rais Samia.
"Jumuiya yetu ya vijana UVCCM wilayani Kishapu, hatupo tayari kuona viongozi wetu wanazungumzwa vibaya, tupo tayari kuwapigania na kukipigania Chama, sisi ndiyo Jeshi la CCM lazima tusimame Imara,"amesema Werema.
Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana UVCCM wilayani Kishapu ukiendelea.
Naye Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, amempongeza Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo Benard Benson Welema kwa utendaji wake kazi, pamoja na kuzunguka Kata zote kuzungumza na Vijana, na kuisemea miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa chini ya Rais Samia.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo.
Amesema Jumuiya ya vijana wilayani Kishapu inaonekana katika viwango vya juu kutokana na uwajibikaji wao, ikiwamo na kuhamasisha viongozi na wananchi kuchangia shughuli za Maendeleo.
Butondo amesema, kazi ya Jumuiya hiyo ya vijana ni kuyasemea maendeleo ambayo yanatekelezwa na Rais Samia, pamoja na kupigania Maslahi ya Chama, kama wanavyofanya UVCCM wilayani Kishapu, na kuwataka waendelee na kasi hiyo na wasirudi nyuma.
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana wilayani Kishapu.
Amesema katika wilaya hiyo ya Kishapu Rais Samia ametoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ambayo inapaswa kusemewa na kuwaziba midomo wapinzani, ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, Madaraja na Makaravati.
Ametaja miradi mingine ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu, Afya, Maji, Umeme ambapo hadi kufikia 2025 hakuna kijiji wilayani humo ambacho hakitakuwa na Nishati ya Umeme.
MBunge wa Kishapu Boniphace Butondo.
Katika hatua nyingine Butondo, amesema UVCCM imekuwa ikitoa viongozi wazuri akiwano nayeye ambaye ni zao la UVCCM, nakuwataka viongozi wachape kazi na kuacha Alama ya kuonekana kwenye utendaji wao kazi, ikiwamo na kujenga Nyumba ya Katibu na kuahidi kuwaunga Mkono.
Pia, amewaonya vijana wasitumike vibaya kisiasa na baadhi ya viongozi ambao ni walafi wa Madaraka na kuanza kuvurugana, na kusema jukumu la vijana kwa sasa ni kulinda viongozi waliopo Madarakani na kukisemea Chama kwa nguvu zao zote.
Amewasihi pia wajumbe wa Mkutano huo, mambo ambayo watayajadili yawe siri yao na siyo kwenda kuyatangaza tena vijiweni, pamoja na kuendelea kuheshimu viongozi wao na wasije wakakisema Chama vibaya.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji, akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Diwani wa Songwa Abdul Ngolomole akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kishapu Benard Benson Werema akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani humo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Kishapu Jamal Namangaya akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (katikati) akiwa na Katibu wa CCM Peter Mashenji (kulia) na Mwenyekiti wa UVCCM Benard Benson Welema kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana wilayani Kishapu.
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana ukiendelea.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (katikati) akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji (kushoto)na Mwenyekiti wa (UVCCM) wilayani Kishapu Benard Benson Werema wakipiga picha ya pamoja.
Viongozi wakipiga picha ya pamoja.
Wajumbe wa Baraza la vijana wilayani Kishapu wakipiga picha ya pamoja na viongozi.
Vijana wa hamasa wilayani Kishapu wakipiga picha ya pamoja.
Awali Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akipokewa na vijana wa hamasa alipowasili kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana wilayani Kishapu kama Mgeni Rasmi ili kufungua Mkutano huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464