HOFU YATANDA DUNIA IKIKUMBWA NA JOTO KALI


Hofu yatanda dunia ikikumbwa na joto kali zaidi kuwahi kutokea


Wimbi kali la joto sasa linaenea kote Amerika Kaskazini na Ulaya. Kuanzia Marekani hadi China na Japan, joto kali limetatiza maisha katika nchi nyingi za Ukanda wa Kaskazini.

 Wataalamu wanaita wimbi hili la joto kuwa 'halikuwahi kutokea'.

Mwezi Juni mwaka huu ulikuwa wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa tangu rekodi za joto duniani kuanza.

Moja ya eneo lilikumbwa na hali mbaya zaidi ya joto kali ni eneo la kusini mwa Mediterania la Ulaya. Halijoto katika bara la Ulaya sasa iko karibu na viwango vya juu zaidi.

Tahadhari zimetolewa kote Italia. Takriban watu 500 wamehamishwa baada ya moto mkali kuzuka katika kisiwa cha La Palma nchini Hispania. Nyumba na magari viliteketea katika moto huko Croatia

Halijoto nchini Ugiriki ilikuwa juu zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya 40 au zaidi siku ya Ijumaa. Acropolis, mojawapo ya vivutio maarufu vya watalii vya Athens, kimefungwa wakati wa msimu wa kilele wa watalii kutokana na joto kali.

Soma hapa zaidi chanzo bbc swahili
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464