HAKI YANGU FOUNDATION, SHY MC WATOA ELIMU YA HOMA YA INI KWA WANAFUNZI CHUO CHA UALIMU SHINYANGA

Afisa Miradi wa Shirika la Haki Yangu Foundation Mkoa wa Shinyanga , Isaac Dumba akielezea lengo la shirika hilo kutoa elimua ya Ugonjwa wa Homa ya ini
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula akitoa elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ini

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Haki Yangu Foundation kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wametoa elimu kuhusu ugonjwa wa Homa ya Ini/ Hepatitis kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa dhidi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 28.

Akitoa elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ini ikiongozwa na kauli mbiu ‘Elimika, Jikinge, Chukua Hatua Sasa, ni haki yako kujua’ leo Alhamisi Julai 27,2023, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula amesema mtindo wa maisha ni miongoni mwa sababu zinazopelekea uwepo wa homa ya ini.

“Mtindo wa maisha ni miongoni mwa sababu zinazochangia uwepo wa homa ya ini na iwapo jamii haitabadilika basi ugonjwa huu utaendelea kuenea kwa kasi mfano ngono zembe, matumizi ya pombe kali. Mtindo wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa homa ya ini kwa mtu binafsi kutokana na kutofuata kanuni na taratibu za afya ”,amesema Mkanula.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula

Mkanula amefafanua kuwa homa ya ini ni ugonjwa unaoletwa na virusi waitwao Hipatisis ambao wamegawanyika katika makundi matano ambayo ni Hepatitis A,B,C,D,na E .

“Hepatitis A na E huambukizwa zaidi kwa njia ya chakula, kama umekula chakula ambacho kina contamination (uchafu), au vinywaji ambavyo vina uchafu, mara nyingi ukizingatia usafi wa chakula, utaweza kujikinga usipate maambukizi ya homa ya ini ambayo ni A na E. Aina nyingine za B,C, na D huambukizwa kwa njia ya maji maji ya mwilini ( body fluids) kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine”,ameeleza.

“Changamoto ya homa ya ini na yenyewe kama ilivyo kwa ugonjwa kama UKIMWI, ukishika damu ambayo ina maambukizo, majimaji ya njia ya uko, kwa njia ya kujamiiana bila kinga na yenyewe pia inaweza kukuambukiza. Tuepuke pia kuchangia vitu vyenye ncha kali na ngono zembe”,ameongeza Mkanula.

Ameeleza kuwa dalili za mwanzo za ugonjwa wa homa ya ini hutokea ndani na miezi 6 baada kuambukizwa virusi vya homa ya ini na kwamba hutokea kwa baadhi ya watu na sio kwa kila mtu ambapo mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini hujiskia kuumwa, upoteza hamu ya kula ,k upata manjano kwenye macho, vinganja vya mikono/kucha au mwili mzima.

Amesema Homa ya ini ni tatizo la kiafya linalohitaji kuzingatia kupima na kufuata maelekezo ya wataalam wa afya katika hatua za kujikinga na ugonjwa huo unaoshambulia ini

“Lengo la serikali ni kuhakikisha inatokomeza ugonjwa wa homa ya ini ifikapo mwaka 2030. Tunawashauri wananchi kupima afya kwenye hospitali mbalimbali ili kujua iwapo wana maambukizo ya homa ya ini ili wataalamu waweze kumpa chanjo, ushauri na hata kuanza matibabu iwapo atabainika kuwa na ugonjwa huo. Ukipima HIV pima pia homa ya Ini”,amesema Mkanula.
Kwa upande wake, Afisa Miradi wa Shirika la Haki Yangu Foundation Mkoa wa Shinyanga , Isaac Dumba amesema shirika hilo lisilo la kiserikali lenye lengo la kuleta maendeleo kisheria, kijamii,kiuchumi na kisiasa kwa wanawake na watoto nchini Tanzania likiwa na dhamira ya uwezeshaji wa mafunzo na ushauri wa kisheria, kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa wanawake na watoto mijini na vijijini limetoa elimu hiyo kwa wanafunzi hao kwani miongoni mwa walengwa ni vijana.

“Miongoni mwa walengwa wa Haki Yangu Foundation ni kundi la vijana ndiyo maana tunakutana na vijana waliopo shuleni na vyuoni na kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali kwani tunataka vijana wapate elimu sahihi. Na katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa dhidi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini tumeona ni vyema tulete elimu ili vijana wapate elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa ini na wachukue hatua”,amesema Dumba.

Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Ualimu waliopata elimu hiyo wamelishukuru Shirika la Haki Yangu Foundation na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuwapatia elimu kuhusu ugonjwa wa homa ya ini huku wakiomba serikali na wadau kupeleka vipimo vya kubaini ugonjwa wa homa ya ini lakini pia kupatiwa chanjo ili kujikinga na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa asilimia 90 ya watu ulimwenguni huishi na ugonjwa wa Homa ya Ini bila kujitambua, huku takribani watu 3000 hufariki dunia kila siku kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya homa ya ini aina hepatitis B na C.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja duniani hupoteza maisha kutokana na maradhi hayo, hatua mbayo mashriika ya afya ulimwenguni,serikali na taasisi zisizo za kiserikali kuanza kutoa elimu kwa jamii wakihamasisha wapime ili kupata chanjo na matibabu ya homa ya Ini.

Hata hivyo WHO inalenga kutokomeza ugonjwa wa homa ya ini ifikapo mwaka 2030 na kunatoa wito kwa nchi kufikia malengo mahsusi ili kupunguza maambukizi mapya ya Hepatitis B na C kwa 90%,kupunguza vifo vinavyohusiana na homa ya ini na saratani kwa 65%, kuhakikisha kuwa angalau 90% ya watu walio na virusi vya hepatitis B na C wametambuliwa.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula akitoa elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ini kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) leo Alhamisi Julai 27,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula akitoa elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ini kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) leo Alhamisi Julai 27,2023. 

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salmon Mkanula akielezea kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ini
Afisa Miradi wa Shirika la Haki Yangu Foundation Mkoa wa Shinyanga , Isaac Dumba akielezea lengo la shirika hilo kutoa elimua ya Ugonjwa wa Homa ya ini
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) wakifuatilia elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya ini
Elimu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya ini ikiendelea kutolewa

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464