Na
Kareny Masasy, Msalala
Halmashauri
ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeendelea kujivunia kwa kuvuka
lengo la ukusanyaji wa mapato na kupata hati safi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 25/07/2025 na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Khamis Katimba kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo nne ya mwaka huku kikiwa na ajenda ya kufanya uchaguzi wa kumpata makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati mbalimbali.
Katimba
amesema ukusanyaji wa mapato utaendelea kusimamiwa vizuri na chama cha Mapinduzi kilimpatia barua yenye jina moja la Mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti ambaye ni Flora
Sagasaga na leo atapigiwa kura kwa kumthibitisha rasmi.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Mibako Mabubu ambaye ameongoza zoezi la kupiga kura kumpata makamu mwenyekiti amesema waliopiga kura ni madiwani 22 na
madiwani wanne hawakuhudhuria baada ya
kuomba ruhusa.
Mibako
Mabubu aliwataja baadhi ya wenyeviti waliochaguliwa kwenye kamati ambapo kamati
ya uchumi,ujenzi na mazingira amechaguliwa Ibrahimu Masanja,kamati ya
Elimu,Afya na Maji amechaguliwa Joseph
Manyara na kamati mbili zimefanyiwa marekebisho ya wajumbe.
Flora
Sagasaga ambaye amekuwa makamu mwenyekiti wa kuchaguliwa tena na madiwani
wenzake amesema anawashukuru madiwani na chama kuendelea
kumuamini zaidi huku akiahidi
kuendelea kupokea ushauri.
Mbunge wa
jimbo la Msalala Idd Kassim amesema
ukusanyaji wa mapato umekuwa mzuri amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kumleta mkurugenzi Khamis Katimba ambaye naye amekuja kwa kasi
kubwa kuhakikisha makusanyo ya fedha yanakwenda vizuri.
Mwenyekiti
wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Thomas Muyonga amesifu ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo huku
akiwashukuru madiwani kupiga kura bila
kelele za kumrudisha makamu mwenyekiti kuongoza tena nakukifanya chama kiendelee kuaminiwa zaidi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu akiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Khamis Katimba akisikiliza hoja kwa umakini
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga akiwashukuru madiwani wenzake kwa kumpigia kura na kushinda tena nafasi ya makamu mwenyekiti
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464