JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA SHINYANGA YALAANI VITENDO VYA UKATILI WANAVYOFANYIWA WATOTO WA KIKE

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na wajumbe wa baraza la jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga

Suzy Luhende,Shinyanga Press Blog

Chama cha Mapinduzi, CCM, kupitia Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga kimelaani vikali vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike ikiwemo tukio la hivi karibuni lililoripotiwa na gazeti la mwananchi la mwanafunzi (16) wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kolandoto kupatiwa ujauzito na mzee wa miaka (65).

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi wakati akifunga kikao cha baraza la wazazi kilichofanyika leo mkoani Shinyanga, ambapo amesema kitendo hicho hakifai katika jamii na kuhimiza mamlaka husika zimtafute na kumkamata mzee huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaoharibu maisha ya watoto wa kike.

"Rais ameleta fedha kwa ajili ya kujenga shule nyingi ili watoto wa kike na wakiume waweze kusoma na kutimiza ndoto zao, lakini wanajitokeza watu wazima wakuharibu watoto wa kike,kama huyu mzee wa miaka 65 aliyempa mimba mwanafunzi inasikitisha sana, hivyo sisi wazazi tusiwe sehemu ya kuharibu watoto wetu, tunaomba vyombo vya dola vimtafute apatikane ili achukuliwe hatua kali za kisheria,"amesema Siagi.

Aidha Siagi amewataka wajumbe wa baraza kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu za kujenga shule ili watoto wote wasome, ambapo pia ni wajibu wa wazazi kusimamia mmomonyoko wa maadili ya watoto na kukemea watu wanaoharibu na kusababisha watoto wa kike wasiendelee na masomo, kila mtu awe mlinzi wa watoto na yanapotokea matukio ya namna hiyo watoe taarifa mapema.

"Hali ya Jumuiya ngazi ya mkoa ni shwari,tunakwenda vizuri na tutazidi kuona mambo mazuri hatujalala tupo tunachapa kazi, mimi mwenyekiti katibu na timu yetu tumeshikamana kama gundi, tunaendelea kufanya mazuri zaidi, nawapongeza sana viongozi wa Jumuiya ya wazazi wilaya kwa kufanya ziara kwani ni sehemu za kuangalia uhai wa Jumuia zetu na CCM tunaendelea kufanya vizuri wilaya zote,. hongereni sana".amesema Siagi.

"Wiki ijayo tunategemea kuanza ziara ya Mkoa mzima ambapo tutatembelea kata zote 130 za Mkoa wa Shinyanga, niombe mkahamasishe viongozi wote wsjitokeze tukakutane nao, wa matawi na kata kwa ajili ya kujenga Jumuiya na Chama chetu,"ameongeza Siagi

Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu amewaomba wajumbe wa baraza la wazazi Mkoa kukemea suala la ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto na ndoa za jinsia moja Ushoga, usagaji na utumiaji wa madawa ya kulevya kwani vitendo hivyo havitakiwi kuendelea kuwepo katika jamii ya kitanzania.

"Jumuiya ya Wazazi inasimamia malezi ya watoto hivyo lazima tushikamane wote tukemee vitendo hivi vya ukatili, ushoga, usagaji,na utumiaji wa madawa ya kulevya ambavyo havina afya kwa Taifa letu la Tanzania, tunatakiwa tuwajenge watoto wetu katika maadili mema wasijiingize kwenye vitendo hivyo"amesema Ndulu.

Aidha katibu amewataka wajumbe wote wa baraza wakasimamie miradi ya maendeleo yote iliyopo katika maeneo mbalimbali wasimwachie mwenyekiti peke yake, wafanye kazi kwa mshikamano ili kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele, na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa kazi anayoifanya ya kuleta maendeleo

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Ally Shaban Majeshi amesema Chama Cha Mapinduzi kina viongozi wa aina mbili kuna viongozi wa kuchaguliwa na viongozi wa kuteuliwa, ambao wote wamepewa dhamana sawa sawa wanatakiwa kuheshimiwa wote.

"Kuna dhana ya kuwashughulikia wale viongozi wa kuteuliwa sio nzuri wengine wanajua kiongozi wa kuteuliwa ni wa kushughulikiwa tu,kwa mfano baadhi ya makatibu wamekuwa wakiingia kwenye kamati za utekelezaji wanakuwa kama wameingia mahakamani wanakuwa kama wahanga wa vikao,kumbe kikao hicho kinatakiwa kumtengeneza katibu ili awe katibu mzuri"amesema Majeshi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na wajumbe wa baraza la jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza na wajumbe wa baraza la jumuiya hiyo
Mjumbe wa baraza la Wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza kwenye baraza la Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga
Katibu Malezi na mazingira Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Bandola  Salum akiwa kwenye kikao cha baraza la Wazazi 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Ally Shaban Majeshi akizungumza kwenye baraza la wazazi Mkoa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na wajumbe wa baraza la jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na wajumbe wa baraza la jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga
Wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga wakiimba na kupiga makofi wakati wakimkaribisha mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa

Mwenyekiti na wajumbe wake wakiendelea na kikao cha baraza
Wajumbe wa baraza la wazazi Mkoa wakimsikiliza Mwenyekiti

Mwenyekiti na wajumbe wake wakiendelea na kikao cha baraza
Wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Shinyanga wakiendelea na kikao
Wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Shinyanga wakiendelea na kikao
Wajumbe wa baraza kabla ya kuanza kikao

Wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Shinyanga wakiendelea na kikao

Wajumbe wa baraza kabla ya kuanza kikao

Wajumbe waniburudika kidogo kabla ya kuanza kikao cha baraza




















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464