Kamati ya maendeleo ya kata ya Tinde, iliyoandaliwa na Chama Cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga,na viongozi wa watu wasiiona wakiwa kwenye picha ya pamoja
Suzy Luhende, Shinyanga SPC blog
Suzy Luhende, Shinyanga SPC blog
Wananchi wa kata ya Tinde wameiomba serikali kuwatengea bajeti ya mafuta ya kuweka kwenye pikipiki za maafisa kilimo ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao, kwa ajili ya kuwapa elimu ya kulima kilimo chenye tija, maana wamekuwa wakishindwa kuwafikia kutokana na kukosa mafuta.
Ombi hilo wamelitoa hivi karibu kwenye mafunzo ya kamati ya maendeleo ya kata ya Tinde, iliyoandaliwa na Chama Cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga, wanaoendelea na mradi wa ufuatiliaji matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za kilimo Mkoa wa Shinyanga kwakutumia kamati ya Public Expenditure Trucking System (PETS).
Mmoja wa wananchi hao Piter Juma waliishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki maafisa kilimo wote wa kata, lakini wanaiomba tena serikali iweke bajeti ya mafuta ya kuweka kwenye pikipiki ili waweze kuwafikia wakulima wote kwa ajili ya kuwapa elimu ya kulima kilimo bora, kwani wakulima wengi hawana elimu ya kilimo wanalima kiholela na kupata mazao kidogo.
"Tunaishukuru sana serikali yetu kwa kuendelea kuongeza bajeti ya kilimo na kutoa pikipiki kwa maafisa kilimo wetu ili waweze kuwafikia wakulima kwa wakati, lakini kuna changamoto ya mafuta wanaweka mafuta kwa fedha yao wanawafikia wakulima wachache na kushindwa kuwafikia wakulima wengi,hali ambayo mkulima anaendelea kulima kilimo kisichokuwa cha tija na kusababisha njaa kila mwaka,"alisema Kabula Masanja.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dickson Maganga kutoka Chama Cha watu wasioona alisema mradi huo ni wa kufuatilia rasilimali za kilimo Mkoa wa Shinyanga, hivyo kamati ya PETS iliyoundwa kufuatilia imefanya ufuatiliaji kwa wananchi na kukuta changamoto hiyo kwamba wakulima hawapewi elimu kutokana na afisa kilimo kukosa mafuta ya kuweza kuwafikia wote.
"Mimi siamini kabisa kama serikali imetoa pikipiki halafu ikakosa mafuta, lazima inatakiwa itengwe bajeti ya mafuta ili kuweza kuwahudumia wakulima angalau wapewe kwa muda furani kuliko kukosa kabisa, ili kuwakomboa wakulima hawa tuombe serikali yetu ilisikie ombi hili ili mkulima aweze kupatiwa elimu ya kilimo bora cha kisasa,"alisema Maganga.
Kwa upande wake diwani wa kata ta Tinde Jafari Kanola amesema ili kuondokana na umasikini wakulima wanatakiwa kupewa elimu na maafisa kilimo ili waweze kubadilika na kulima kilimo cha kisasa, na kwa sababu amesikia wanauhitaji wa mafuta hawapatiwi kutoka halmashauri atalifikisha kwenye vikao vya baraza ili halmashauri iweze kutenga bajeti ya mafuta.
"Mimi ndo nasikia leo kwamba maafisa kilimo hawajatengewa bajeti ya mafuta kwa vile nimesikia na nimwakilishi wa wananchi nitaenda kulizungumza kwenye kikao cha baraza ili wataalamu hawa waweze kupatiwa mafuta na wawafikie wakulima kwa wakati na kuwahudumia"alisema Kanola.
Tuone umuhimu mradi huu uliokuja kwa ajili ya kutusaidia , tushirikiane katika kufuatilia rasilimali za kilimo tuangalie kama huduma kwa mkulima zinatolewa ipasavyo na maafisa kilimo, lakini kutokana na changamoto ya mafuta tumeshalijua tutalifikisha ili liweze kutatuliwa,"ameongeza Kanola.
Afisa kilimo wa kijiji cha Nyambui kata ya Tinde Edmund Kinubi amesema wananchi wa kata ya Tinde wanategemea kilimo, lakini bado kilimo hatujakitendea haki na hakijapewa uzito, serikari inatoa mbolea za ruzuku na wanatakiwa wakulima wajiandikishe kulingana na heka wanazolima ili isiwe usumbufu siku ya kupelekewa mbolea.
"Utaratibu wa mbolea serikali imesema itajitahidi kuwasogezea karibu mbolea na wataangalia maghala yenye sifa na watapeleka hapo kwa wakati ili ziweze kuwafikia kwa wakati wakulima,"amesema Kinubi.
Mratibu wa mradi huo Agness Makambajeki amesema mradi huo unaendeleana utadumu kwa miezi mitano umeanza mwezi wa sita unaishia mwezi wa 10, hivyo wameomba ushirikiano ili kujua wapi kunachangamoto ili ziweze kutatuliwa.
Mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa aliwaomba viongozi wa kamati ya maendeleo kushirikiana vizuri na kamati ya PETS amabayo imeundwa kwa ajili ya kufuatilia rasilimali za umma za kilimo ambao wanakamati hao wamechaguliwa na wananchi wa kata ya Tinde
Kamati ya maendeleo ya kata ya Tinde, iliyoandaliwa na Chama Cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga,ikiendelea kupatiwa mafunzo
Kamati ya maendeleo ya kata ya Tinde, iliyoandaliwa na Chama Cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga,ikiendelea kupatiwa mafunzo
Mwenyekiti wa mradi wa ufuatiliaji rasilimali za umma za sekta ya kilimo Marco Nkanjiwa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Diwani wa kata ya Tinde Jafari Kanola ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo kata hiyo akizungumza
Katibu wa watu wasioona Mkoa wa Shinyanga Agness Makambajeki baye pia no mratibu wa mradi wa ufuatiliaji rasilimali za umma za sekta ya kilimo
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya maendeleo akizungumza kwenye mafunzo ya kamati ya maendeleo
Mwezeshaji wa mafunzo kutoka chama cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga Dickson Maganga akitoa maelekezo
Kamati ya maendeleo ya kata ya Tinde, iliyoandaliwa na Chama Cha watu wasioona Mkoa wa Shinyanga,na viongozi wa watu wasiiona wakiwa kwenye picha ya pamoja