MADINI YAPONGEZWA KWA KUTOA ELIMU NA KAMPUNI YA GGML


*#GGML wapongeza Mkaa mbadala wa STAMICO

*#GGML Kinara uchangiaji huduma kwa jamii


Wizara ya Madini imepongezwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kutoa elimu kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda la Wizara, taasisi zake na wadau wa Sekta ya Madini.

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 11, 2023 na Mwanasheria Mkuu wa kampuni ya GGML David Nzaligo alipotembelea banda la Wizara ya Madini (MADINI PAVILION) katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.


Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Nzaligo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuleta Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes ambao utasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Akiwa katika banda la kampuni ya GGML ambalo lipo pia ndani ya banda la madini, Nzaligo amewapongeza wafanyakazi wa GGML na kampuni zingine ndani ya banda hilo kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kutoa elimu ya shughuli wanazozifanya ikiwemo uchimbaji madini na mnyororo wake.

"Nafahamu GGML wapo vizuri kwenye miradi mingi ya kijamii pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Nafurahi kwamba mafanikio hayo wanayaelezea vizuri kwa kila mwananchi anayetembelea banda la GGML," alisema.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464