Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akijiandaa kukata utepe kwaajili ya uzinduzi wa mtandao wa maji vijiji vya Nyamilangano.
Na Kareny Masasy,
Ushetu
MWENGE wa Uhuru
umezindua mtandao wa maji utakao wanufaisha
wananchi zaidi ya 5200 wa vijiji vya Mitonga na Ididi kata ya Nyamilangano halmashauri ya Ushetu
wilayani Kahama Mkoani Shinyanga uliotekelezwa na Wakala wa Maji safi na Mazingira vijijini (Ruwasa).
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amezindua leo tarehe 31/07/2023 katika Mtandano huo wa maji chanzo chake ni kisima kirefu ambao umegharimu sh Millioni 229.7.
Kaim amesema kupitia program ya malipo kwa matokeo imefanya upanuzi wa mtandano wa maji na kuangalia idadi ya watu na uhitaji ni kuhakikisha wananchi wanapata maji na kuwataka waunganishe mahitaji yao.
“Vyanzo hivi vya maji vinatakiwa kulindwa na kuhifadhiwa vizuri ili viweze kuwanufaisha wananchi wote kama ilivyokusudiwa serikali ya awamu ya sita inachotaka nikuwapatia huduma wananchi wake”amesema Kaim.
Akisoma taarifa hiyo meneja wa Wakala wa maji Safi na Mazingira vijijini (Ruwasa) wilaya ya Kahama Paschal Mnyeti amesema mradi huu umeongeza huduma ya maji kwa kata ya Nyamilangano kwa upatikanaji wa maji asilimia 75.
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani amesema Ushetu inauhitaji wa huduma ya upatikanaji wa maji ikiwa usanifu umefanyika katika maeneo mbalimbali ili kuweza kupata maji ya ziwa Victoria.
Wakijiandaa kupokea mwenge wa Uhuru halmashauri ya Ushetu.
Mradi wa maji uliotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)
Mradi wa maji
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdalla Kaim akijiandaa kukata utepe kwaajili ya uzinduzi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464