MWENGE WA UHURU UMEZINDUA,KUONA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI MANISPAA KAHAMA



Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizundua sekondari ya Kagongwa iliyopo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Na  Kareny  Masasy,

Kahama

KIONGOZI wa mbioa za Mwenge wa Uhuru Kitaifa   2023 Abdalla  Shaib Kaim ameweza kuona  ujenzi wa jengo la uchunguzi wa magonjwa mbalimbali  katika hospitali ya manispaa ya Kahama  mkoani Shinyanga

 Ikiwa  jengo hilo limekamilika kwa asilimia 100  na limetekelezwa  na mkandarasi SUMA JKT Costruction  Co. Ltd chini ya usimamizi  wa Mhandisi  wa halmashauri  kwa kutumia Force Account.

Akisoma taarifa  leo tarehe 30/07/2023  mbele ya kiongozi huyo juu ya mikakati ya kuanza kwa jengo hilo  mganga mkuu wa manispaa ya Kahama Joesphat Shani amesema  ujenzi ulianza mwezi Februari mwaka jana (2022) kwa lengo la kuwa na kituo cha vipimo vya uchunguzi vya kisasa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa  Kaim ameona jengo hilo nakuwapongeza manispaa ya Kahama kwa kuongeza kutumia mapato ya ndani ingawa na serikali kuu nayo imechangia kwa lengo la kutaka huduma kuwepo karibu kwa wananchi wake.

“Juhudi za serikali ya awamu ya sita  kwa kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan nikutaka kuona  watu wake wanaendelea kuwa na afya bora ndiyo maana anaboresha  huduma za afya”amesema Kaim.

Pia kiongozi huyo amezindua ofisi ya kata ya Nyihogo na kupanda miti kwa kushirikiana na wananchi wa manispaa ya Kahama

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita baada ya kuwasili mwenge  amesema mwenge wa Uhuru kwa manispaa ya Kahama  utazindua,kuona na kuweka mawe ya msingi  katika miradi sita.



Jengo la  uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ambalo kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa  ameliona.



Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa akipanda mti eneo lililotengwa katika kata ya Nyihogo.

Kiongozi akipanda mti eneo la Nyihogo kwaajili ya kutunza mazingira

Mbunge viti maalum  Santiel Chilumba  akipanda mti kutunza mazingira 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama  Anderson Msumba akijiandaa kupata mti eneo la Nyihogo.

Jengo la uchunguzi wa magonjwa mbalimbali

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimkabidhi mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Kahama  Mboni Mhita  ambapo utakimbia wilaya ya Kahama kilomita 258.1


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464