Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Hadija Mohamed akijiandaa kupokea mwenge wa Uhuru katika halmashauri hiyo baada ya kukabidhiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba.
Na Kareny Masasy,
Ushetu
MWENGE wa Uhuru umeweza kuona,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita ya halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga yenye thamani ya Sh Millioni 920 na umekimbizwa kilomita 99.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdalla Shaib Kaim leo tarehe 31/07/2023 ameweka jiwe la msingi vyumba vya madarasa vitano vilivyogharimu sh Millioni 101 katika shule ya msingi Ukune na Zahanati ya kijiji cha Igalula kilichogharimu sh Millioni 81.
Pia kiongozi huyo ameona ujasiliamali kwa wanawake wanaoishi katika kijiji cha Mpunze (Mpunze Industry Group) ambapo wanafanya shughuli za kusaga nakukoboa nafaka za mahindi na Mchele ambayo ilipatiwa mkopo na halmashauri ya Ushetu ya asilimia 10.
Abdalla Shaib Kaim ameweka jiwe la msingi kwenye nyumba ya mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu iliyojengwa kwa gharama ya sh Millioni 150 mpaka kukamilika kwake.
“Serikali imetoa fedha hizi kwa kuhakikisha watu wake wanaishi katika mazingira bora kila kukicha Rais Samia Suluhu Hassan anahangaika kutafuta fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo”amesema Kaim.
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani amesema ujenzi wa Zahanati ulianza mwaka 2016 kupitia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan umetoa fedha za kukamilisha Zahanati hiyo.
Mkuu wa wilaya Kahama Mboni Mhita amesema serikali inawajali kwa kuwapatia miradi mbalimbali kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi wake upande wa shule ya msingi Ukune licha ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa imekarabatiwa majengo yake mengine.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464