Ndoto za Magufuli Uwanja wa Ndege Chato
Miongoni mwa majengo ya Uwanja wa Ndege Chato.
Maskini uwanja wa ndege wa Chato! Hata kampuni moja ya ndege iliyokuwa inakwenda Chato, mara moja kwa wiki, sasa imesimamisha safari zake.
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Sarah Reuben akijibu swali la Mwananchi “kwa nini safari za Chato zimefutwa,” anasema “hazijafutwa” isipokuwa kuna mabadiliko katika mpangilio wa safari kwenye viwanja kadhaa.
“Kutokana na baadhi ya ndege zetu kupaki (kuwa katika matengenezo), tumepunguza safari katika baadhi ya viwanja (njia) na sio kwamba tumesitisha,” anasema Reuben alipoulizwa na Mwananchi Juni 21.
Anafafanua kuwa hatua hiyo inatokana na mahitaji ambapo baadhi ya viwanja vimeongezewa safari.
Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464