PROGRAM JUMUISHI YA MALEZI NA MAKUZI YATAMBULISHWA KWA WADAU-SHINYANGA
Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Shinyanga,Nuru Mpuya akitoa maelezo kwa washiriki juu ya program ya malezi.
Na Kareny Masasy,
Shinyanga
Wadau mkoani Shinyanga wametambulishwa programu jumuishi ya Taifa ya malezi makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJ T-MMMAM) ili kuweza kutambua maendeleo ya ukuaji wa Mtoto tangu umri 0 hadi miaka 8.
Utambulisho huo umetolewa leo tarehe 20/07/2023 na ofisa maendeleo ya jamii Tedson Ngwale akishirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii mkoa Lyidia Kwesigabo kwenye kikao cha wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana ,makao makuu ya yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Ngwale amesema watoto wanatakiwa kufanyiwa maandalizi tangu kutungwa kwa mimba hadi miaka minane ambapo ndicho kipindi ambacho ana utayari wa kujifunza anachokisikia,kuona na kujaribu matendo mbalimbali.
Ngwali amesema mama mwenyewe anaoushahidi wa mtoto anapotaka kujifunza baada ya kuzaliwa hasa hufuata inshara Kama mawasiliano kwake na matumizi ya lugha kufahamu neno mojamoja kinachotakiwa ni kuwa makini katika muendelezo wa makuzi ya mtoto katika matamshi yasiyo na staha.
"Vikwazo vinavyowakumba watoto katika ukuaji ni lishe duni, ukatili msongo wa mawazo,umasikini "amesema Ngwale.
Ngwale amesema kuna dhana tano muhimu ambazo mtoto anatakiwa kuzipitia kadri ya ukuaji wake ambapo kuna afya,lishe,ujifunzaji wa awali na malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.
Mgeni rasmi katika utambulisho wa programu hiyo ambaye ni kaimu mganga mkuu wa mkoa dk Nuru Mpuya akimwakilisha katibu tawala mkoa amesema vituo vya kulelea watoto mchana lengo kuu ni kutoa huduma zinazoelezwa kwa mujibu wa muongozo wa wizara zilizoainishwa ikiwemo afya na lishe.
Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo amesema vituo vinapoomba usajili vinaeleza kukidhi vigezo upande wa chakula na watoto walionao changamoto iliyopo hawafanyi hivyo matokeo yake kuwapatia chakula cha aina moja kutwa nzima.
Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamis amesema udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ni changamoto ambapo umri huo wako kwenye vituo vya kulelea watoto inatakiwa wapewe vyakula vyenye virutubisho ili kuondokana na changamoto ya udumavu.