Diwani wa kata ya Sabasabini Emanuel Makashi akihesabu kura baada ya kupata kura zote za ndiyo kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu.
Na Kareny Masasy,Ushetu
MADIWANI wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamemchagua Emanuel Makashi diwani wa kata ya Sabasabini kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo huku akitoa ujumbe mzito .
Ambapo Makashi amechaguliwa leo tarehe 24/08/2023 na madiwani 26 waliopiga kura za ndiyo huku mwenyekiti wa halmashauri hiyo Gagi Lala akimtangaza nakumkaribisha katika kiti hicho.
Makashi amewashukuru madiwani wenzake kwa kumchagua nakueleza anachotaka ni ushirikiano “ Gari lisiachwe mpaka likapinduka ndiyo utolewe ushauri bali utolewe kwanza ushauri kunusuru maisha ya abiria”….. na uongozi haujabadilika ni uleule.
“Hiki kiti ni chakupokezana mwaka jana nilimkabidhi diwani Doa Limbu nafasi ya makamu mwenyekiti na leo amenirudishia tena kushika nafasi hii hivyo mwenzangu mlimpatia ushirikiano wakutosha na mimi napenda iwe hivyo ”amesema Makashi.
Doa Limbu ambaye ni diwani wa kata ya Nyankende ameshukuru kwa kipindi chote alichokaa nakushirikiana vizuri huku akieleza ukusanyaji wa mapato aliusimamia vizuri ikiwemo miradi inayotekeleza na fedha kutoka serikali kuu.
Sisi madiwani tunatakiwa tuwe walezi wa usimamizi wa fedha katika idara zote ili miradi iweze kutekelezwa kwa viwango na wananchi wanufaike katika suala la ukusanyaji wa mapato tunatakiwa kwa mwezi tufikie asilimia 8.3 ili tulifikie lengo la asilimia 100.
Aidha katika uchaguzi huo zilichaguliwa kamati mbalimbali ambapo kamati ya Elimu,afya na Maji alichaguliwa Doa Limbu kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo huku kamati ya Uchumi,ujenzi na Mazingira alichaguliwa Kulwa Shoto kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo huku Yohana Mande akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili.
Katika kikao hicho kilichokuwa na ajenda sita mkurugenzi wa halmashauri hiyo Hadija Mohamed aliwataka madiwani kuangalia namna ya ratiba ya vipindi vya vikao kwa mwaka wa 2023/2024.
Diwani wa kata ya Sabasabini Emanuel Makashi akishukuru kwa kumchagua kuwa makamu mwenyekiti.
Mwenyeviti wa kamati za mbalimbali wakijiandaa kujiuzuru kamati hizo
Diwani wa kata ya Nyankende Doa Limbu akijiuzulu nafasi ya makamu mwenyekiti kwa kujiandaa kumpigia kura makamu mwenyekiti aliyepitishwa..
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Hadija Mohamed akisoma ajenda za kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Diwani wa kata ya Sabasabini Emanuel Makashi akijieleza kwa madiwani wenzake nakuomba kura nafasi ya makamu mwenyekiti wa halmashauri.
Mdiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza
Diwani Emanuel Makashi akihesabu kura.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gagi Lala akifungua kikao cha baraza la madiwani.