RC MNDEME AHIMIZA AKINA MAMA UNYONYESHAJI WATOTO,LISHE BORA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewahimiza akina mama mkoani humo, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa Afya katika suala zima la unyonyeshaji watoto maziwa ya mama pamoja na lishe bora, ili wakue kimwili na kiakili.
Amebainisha hayo leo Agosti 5, 2023 kwenye Maadhimisho ya siku ya Lishe na wiki ya unyonyeshaji Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Amesema maziwa ya mama kwa watoto wadogo yana virutubisho pamoja na kinga ya mwili, ambayo yataimarisha Afya yake na kumuepusha na maradhi ya mara kwa mara.
“Mtoto akizaliwa baada ya saa moja, anapaswa kunyonyeshwa na anyonyeshwe yale maziwa ya kwanza ya njano na siyo kuyakamua na kuyamwaga yanavirutubisho tosha kabisa na hayana madhara,”amesema Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akigawa uji wa lishe kwa watoto.
“Mtoto pia anapaswa kunyonyeshwa ndani ya miezi sita bila kupewa chakula chochote wala maji, na wakati ukifika wa kumpatia vyakula vya ziada lizingatiwe suala la lishe bora huku akiendelea kunyonyweshwa hadi afikishe miaka miwili,”ameongeza.
Aidha, amewataka pia waajiri wa sekta binafsi kutoa fursa kwa wafanyakazi ambao wamejifungua watoto, wawe na muda wa kunyonyesha watoto wao na kutengewa chumba maalumu kwa ajili ya kumhudumia mtoto wake, sababu maziwa ya mama ni kinga bora na kupungua pia tatizo la udumavu na utapiamlo na vifo vya watoto wachanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa amembeba mtoto mwenye Afya njema ambaye amenyonyeshwa maziwa ya mama.
Katika hatua nyingine amesema tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Shinyanga limepungua, kutoka asilimia 32.1 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 27.5 mwaka 2022.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amewasisitiza akina mama kuendelea kuzingatia ushauri wa wataalamu wa Afya katika suala zima la unyonyeshaji na lishe bora ili kuwakinga na maradhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Afisa lishe Mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamisi, amesema ni asilimia 30 tu ya akina mama katika Mkoa wa Shinyanga ambao wananyonyesha watoto wao ndani ya saa moja baada ya kujifungua, na kuwasisitiza kuwa maziwa ya mama kwa mtoto ni muhimu sana katika afya yake na ukuaji kimwili na kiakili.
Amewasihi pia akina mama wazingatie suala la lishe bora kwa watoto wao kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula.
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamisi.
Nao baadhi ya akina mama akiwamo Kareny Jamsoni, ametoa ushuhuda kwa wanawake wenzao, namna walivyozingatia suala ya unyonyeshaji kwa mtoto wake ndani ya miezi sita bila ya kumpatia kitu chochote kile cha kula na sasa ana Afya njema.
Kareny Jamsoni.
Kauli Mbiu katika maadhimisho hayo inasema”saidia unyonyeshaji, wezesha wazazi kulea watoto na kufanya kazi zao kila siku.”
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Diwani wa Ndala Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Mwanamke Khadija Brayson akitoa ushuhuda namna alivyo mnyonyesha Mtoto wake ndani ya miezi sita bila ya kumpatia kitu chochote cha kula na sasa ana Afya njema.
Afisa Lishe Manispaa ya Shinyanga Amani Mwakipesile akitoa elimu ya lishe bora kwa kuzingatia makundi matano ya chakula.
Akina mama wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya lishe na wiki ya unyonyeshaji.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipima Shinikizo la damu kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akipima shinikizo la damu kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kugawa uji wa lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akigawa Bokoboko yenye lishe bora kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiendelea kugawa Bokoboko yenye lishe bora kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na RMO Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile wakigawa Bokoboko yenye lishe bora kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akinywa uji wa lishe.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akinywa uji wa lishe.
Mganga Mfawidhi wa Manispaa ya Shinyanga Dk. Elisha Robert akinywa uji wa lishe.
Diwani wa Ndala Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akinywa uji wa lishe
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa amembeba mtoto ambaye amenyonya maziwa ya mama na kuwa na Afya njema.