FADev imetoa vifaa kinga kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
TAASISI ya kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini (FADev)imetoa vifaa kinga kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Machimbo ya Ntambalale wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, ili kuwakinga na madhara mbalimbali katika shughuli zao za uchimbaji madini.
Vifaa hivyo vimetolewa jana na FADev kwa ufadhili wa Shirika la SWISSAID.
Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, (kushoto) akikabidhi vifaa kinga kwa Mwenyekiti wa Mgodi wa Isanja ndugu Gold Mine Hamis Mabubu.
Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Mhandisi Theonistina Mwasha, amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini juu ya kuzingatia Afya na usalama wao kazini, hivyo wakaona ni vyema sasa kuwapatia na vifaa kinga ambavyo vitawakinga na madhara mbalimbali katika uchimbaji huo wa madini.
Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha.
“Vifaa kinga ambavyo tumevitoa ni viatu vya usalama (safety boot) Kofia ngumu, Maski,Miwani, Groves,Koti za kuaksi mwanga (Leflector) hasa wanapokuwa chini ya mashimo, na vifaa vya kuziba masikio,”amesema Mhandisi Mwasha.
Aidha, amesema matarajio ya FADev ni kuona wachimbaji wadogo wa madini wanafanya shughuli zao za uchimbaji huku wakibaki kuwa salama, na kuacha kufanya shughuli hizo kimazoea na kuathiri Afya zao.
Naye Mchimbaji Mdogo wa dhahabu katika Mgodi wa Isanja ndugu uliopo eneo la Machimbo ya Ntambalale Anthony Thomas, amesema wachimbaji wengi hawana elimu ya usalama wao, na wamekuwa wakifanya shuguli hizo kimazoea na hupata madhara ya mara kwa mara kutokana na kutovaa vifaa kinga.
Mchimbaji mdogo wa dhahabu Anthony Thomas akipasua miamba huku akiwa amevaa vifaa kinga.
“Vifaa kinga ni muhimu sana katika shughuli zetu hizi za uchimbaji madini, ukiangalia mikono yangu nimejiponda sana na hata chembechembe za miamba huingia kwenye macho yetu, tunashukuru kupata elimu ya usalama na vifaa kinga,”amesema Thomas.
Mwenyekiti wa Mgodi wa Isanja ndugu Gold Mine Hamis Mabubu, amesema vifaa kinga ambavyo wamepewa na Taasisi hiyo ya FADev watavitumia kwa madhumuni yaliyotarajiwa na vikichakaa watanunua vingine kwa ajili ya kuwalinda wachimbaji sababu wameshapata elimu ya Afya na usalama kazini.
Mchimbaji mdogo wa Madini ya dhahabu Sebastian Lucas akiwa amevaa vifaa kinga wakati akiingia dani ya shimo kuchimba madini.
Migodi midogo ambayo imepewa vifaa kinga na FADev ni Isanja ndugu Gold Mine, na Ntambalale namba 4 ambayo ipo wilayani Kahama, pia ilitoa vifaa hivyo katika migodi mingine ya Geita ambayo ni Mgusu, Nsangano,Rwamgasa, Ushirika Mgusu, na Nyarugusu.
Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, (kushoto) akikabidhi vifaa kinga kwa Mwenyekiti wa Mgodi wa Isanja ndugu Gold Mine Hamis Mabubu.
Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, (kushoto) akikabidhi vifaa kinga kwa Mwenyekiti wa Mgodi wa Isanja ndugu Gold Mine Hamis Mabubu.
Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, (kulia) akikabidhii Vifaa kinga wa uongozi wa Mgodi wa Ntambalale namba 4.
Muonekano wa Vifaa kinga Safety Boot.
Katibu Mtendaji na Mchimbaji katika Mgodi wa Isanja ndugu Gold Mine Emmanuel John akielezea umuhimu wa kuvaa vifaa kinga katika shughuli za uchimbaji madini.
Muonekano wa vifaa kinga kofia ngumu.
Mwanamke Mchimbaji wa Madini Dotto Kilalo akielezea umuhimu wa kuvaa vifaa kinga Migodini.
Muonekano wa vifaa kinga vya kuvaa masikioni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464