Presha ya uchaguzi yaanza kupanda
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga.
Dar es Salaam. Ulikuwa mjadala wa kupeana ‘makavu’ kwenye mkutano wa wadau wa siasa nchini kuhusu hali ya demokrasia, hali iliyoonyesha wazi kuwepo presha ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu 2025.
Katika mkutano huo ulioanza Agosti 22, 2023 ma kuhitimishwa jana Agosti 23, 2023 hoja nyingi zilielekezwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara), Abdulrahman Kinana aliyekuwepo kukiwakilisha chama hicho.
Miongoni mwa hoja hizo ni madai kuwa CCM ndiyo sababu ya kudorora kwa mchakato wa Katiba mpya na wengine wakitaka hakikisho la kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi unaofuata.
Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464