KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA KILOLELI WILAYANI KISHAPU KIMECHANGIA KUANZISHWA UJENZI WA MATUNDU 24 YA VYOO SHULE YA MSINGI KUNUSURU AFYA ZA WANAFUNZI
Na Kareny Masasy,
KISHAPU.
WANANCHI wa kijiji cha Kiloleli halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga kupitia kituo cha taarifa na Maarifa, wameanzisha ujenzi wa matundu ya vyoo 24 pamoja chumba kimoja cha wanafunzi wa kike kwa ajili ya kujistili na hedhi na kunusuru Afya za wanafunzi baada vyoo katika shule hiyo kuwa katika hali mbaya na havitumike na kulazimika wanafunzi kujisaidia vichakani.
Vituo vya taarifa na maarifa zimekuwa zikijengewa uwezo na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) namna ya kuibua changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili jamii na kuzitafutia ufumbuzi.
Muonekano wa choo cha zamani.
Wanakituo cha taarifa na maarifa wakiongea na waandishi wa habari jana ambao walitembelea kijijini humo ili kuona changamoto ambazo waliziibua na kisha kuzitafutia ufumbuzi, wamesema kuna vitu vingi ambavyo wameviibua na wameanza kuvitafutia ufumbuzi moja baada ya kingine.
Mmoja wa wana kituo hao Helana Makelele amesema wanafunzi katika shule ya msiingi Kiloleli, wamekuwa wakijisaidia vichakani baada ya matundu ya vyoo manane kujaa na hayatoshelezi kwa wanafunzi waliopo wakahamasishana wao na baadaye kulipeleka kwenye Mkutano wa hadhara wananchi wakakubali kuchangia fedha.
Mwanakituo cha taarifa kijiji cha Kiloleli Helena Makelele.
Mwanakituo cha taarifa na Maarifa kutoka Kiloleli Joseph Solea amesema waliona changamoto kubwa ni kukosa matundu ya vyoo maana yaliyopo yalikuwa yamejaa wakajadiliana walihamasisha na jamii ikawakubali kuanza kutoa sh 1000 na kuchimba shimo kwa kujitolea na wakaona haitoshi wakarudi tena kuchangia sh 2000 wanafunzi wakihitaji huduma wanajitafutia mahali popote.
Mwanakituo cha Taarifa na Maarifa kutoka Kiloleli Joseph Solea.
Mkazi wa kijiji cha Kiloleli Martha Ngwelu amesema waliibua ujenzi wa vyoo kutokana na vyoo vyenye matundu manane kujaa na havikutosheleza kutokana na idadi ya wanafunzi hivyo waliitishwa mkutano wa hadhara na kukubaliana kuanzisha ujenzi huo.
Muonekano wa matundu ya choo ambayo yanajengwa na kituo cha Tarifa na Maarifa kutoka Kata ya Kiloleli wilayani Kishapu.
“Hamasa ilitoka kwa wanakituo cha taarifa na maarifa baada ya wao kuanzisha harambee ya mchango na kutoa sh 50,000 na mifuko ya Saruji mitano lakini sisi mara nyingi tulikuwa tukiliongelea kwenye mikutano ya hadhara bila mafanikio wao wametuhamasisha vyoo vimeanza kujengwa”amesema Ngwelu..
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kiloleli Juliana Petro amesema shule hiyo ina wanafunzi 997 changamoto iliyopo ni ukosefu wa matundu ya vyoo na wanafunzi wanapitwa na masomo kwa kushelewa chooni sababu ya matundu yaliyokuwepo yamejaa na machache na sasa wanajisaidia vichakani.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kiloleli Juliana Petro.
“Matundu 24 ya vyoo yaliyojengwa yatasaidia kuondoa changamoto iliyokuwepo awali kulikuwa hakuna chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike sasa kimewekwa jamii imeanza kupata uelewa kwani uwiano unaotakiwa wanafunzi 25 tundu moja kwa wakiume na wakike wanafunzi 20 tundu moja”amesema Petro.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kiloleli Kuhwema Mshala amesema changamoto zilizokuwepo shuleni matundu ya vyoo yalikuwa hayatoshi na yamejaa wakaamua kuwaita vituo vya taarifa na maarifa na wananchi wakazungumza kwenye mkutano wa hadhara na kukubaliana kituo cha taarifa na maarifa kutoa sh 50,000 na Mifuko ya Saruji Mitano.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kiloleli Kuhwema Mshala.
“Wananchi walikubaliana kuchangia sh 2000 tukanunua nondo na Saruji na kujenga bamba na wananchi wakachimba tena karo na kuleta mchanga nguvu kazi na kikao cha Maendeleo ya kata (WARDC) walitoa mifuko 30 ya Saruji na matofali yakavyatuliwa kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo”
Mashara amesema serikali ya kijiji ilitoa sh 600,000 na Sungusungu walitoa sh 500,000 na ujenzi ukaanza na wanaiomba serikali waongeze fedha waweze kupaua lakini wakiona wanachelewa watajitahidi wakamilishe wenyewe.
Mtendaji wa kijiji Nicholaus Mzirai amesema halmashauri ya kijiji hicho wamepata Sh millioni 1.3 zitokanazo na ushuru wa zao la pamba na wamefanya matumizi ya sh 500,000 kwaajili ya uendelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo na michango ya wananchi ilipatikana sh 700,000.
Mtendaji wa kijiji Nicholaus Mzirai, akizungumzia ujenzi wa matundu ya vyoo.
Muonekano wa choo cha zamani shule ya msingi kiloleli.
Muonekano wa choo cha zamani shule ya msingi kiloleli.
Muonekano wa choo cha zamani shule ya Msingi Kiloleli wilayani Kishapu.
Muonekano wa matundu mapya ya choo katika shule ya Msingi Kiloleli ambayo yanajengwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kiloleli wilayani Kishapu.
Muonekano wa Matofali ambayo wanafyatua kujenga Matundu hayo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464