WADAU WAPONGEZA MATOKEO YA UTAFITI KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA SHINYANGA


WADAU WAPONGEZA MATOKEO YA UTAFITI KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WADAU wa Maendeleo mkoani Shinyanga, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga dhidi ya wanawake na watoto, wamepongeza matokeo ya utafiti wa kutokomeza ukatili ndani ya jamii.

Wametoa pongezi hizo leo Agosti 16, 2023 wakati Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) na Shirika la Citizen For Change, walipokuwa wakiwasilisha matokeo ya utafiti dhidi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga, utafiti ambao umefanyika ndani ya miaka miwili katika Kata 18 wilayani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano.

Wakizungumza wakati wa kutoa maoni yao juu ya utafiti huo, wamesema vitu ambavyo vimeanishwa dhidi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii vipo sawa, sababu jamii imehusishwa moja kwa moja na kutengeneza mbinu saba ambazo zitatumika kupambana na ukatili huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Mkutano huo, ameishukuru WFT kwa kutoa Ruzuku na kutekelezwa miradi ya ukatili wilayani humo, hali ambayo imeleta mabadiliko makubwa ndani ya jamii na kupunguza vitendo vya ukatili.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje.

“Kazi ambayo mnaifanya WFT ni kazi iliyopaswa kufanywa na Serikali, hivyo tunawashukuru kwa kazi nzuri ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, na tangu miradi hii ianze kutekelezwa mabadiliko tumeyaona,”amesema Mboje.

Afisa Program Mwandamizi kutoka WFT-Trust Neema Msangi, amesema utafiti huo wameufanya Mkoani Shinyanga kama eneo la kujifunza, na umefanyika katika Kata 18 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na wameishirikisha jamii husika ili kujadili nini kifanyike kumaliza ukatili.
Afisa Program Mwandamizi kutoka WFT-Trust Neema Msangi.

Mkuu wa Idara ya ukuzaji Rasilimali na Mawasiliano kutoka (WFT) Carol Mango, amesema utafiti huo umefanyika kwa miezi 21 sawa na miaka miwili kuanzia 2021 hadi 2023, kwa kushirikiana na Shirika la Citizens for Change ambao ndiyo walikuwa watekelezaji wa utafiti huo, na WFT ni watoaji wa Ruzuku.

Amesema kupitia utafiti huo pia wamebaini kwamba mifumo isiyo rasmi, imekuwa ikiaminika sana na jamii katika kupambana na ukatili, na ndiyo wamekuwa wakipewa taarifa za ukatili tofauti na mifumo ambayo ni rasmi ambao wao ndiyo watoa maamuzi.
Mkuu wa Idara ya ukuzaji Rasilimali na Mawasiliano kutoka (WFT) Carol Mango.

“Lengo la utafiti huu ni kujifunza pamoja na kuishirikisha jamii na kuwa na nguvu ya pamoja na kubaini mbinu ambazo zinaweza kutumika katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii,”amesema Mango.

Naye Mathias Mkude kutoka Citizen for Change na TICD akiwasilisha matokeo ya utafiti, amesema utafiti huo wahusika wenyewe ambao ni wanabadiliko ngazi ya jamii (Backbone) walihusika kutengeneza mbinu saba ambazo zitasaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia, kuwa ni kufufua vikao vya familia nyakati za usiku (Shikome) ambavyo licha ya kujadili masuala ya kifamilia pia vitatumika katika mazungumzo ya kupinga ukatili.

Ametaja Mbinu zingine kuwa ni kuhamasisha viongozi na Walimu Wakuu kuelimisha walimu kuhusu masuala ya ukatili, kuhamasisha viongozi wanawake na watoto kuhudhuria kwenye Mikutano ya kijiji na kutoa maoni yao dhidi ya kupambana na ukatili.
Mathias Mkude kutoka Citizen for Change na TICD.

Pia kupitia Mikutano hiyo itumike kupitisha Sheria ndogo ambazo zitasaidia kupambana na ukatili, kushawishi viongozi Kata na vijiji kutoa adhabu kali kwa watu ambao wanaendekeza ukatili, kuwezesha midahalo ya kijamii kujadili namna ya kuzuia ukatili, pamoja na kutungwa sheria kali kwa wazazi ambao wanabagua watoto na kutowapeleka shule.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Rehema Edson, amesema utafiti huo ukawe chachu ya kuongeza juhudi katika mapambano ya ukatili, na kuifanya jamii ibakuwa kuwa salama hasa wanawake na watoto ambao ndiyo waathirika wakubwa wa ukatili.
Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust)Glory Mbia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Rehema Edson akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Ntomela akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo wa Matokeo ya utafiti dhidi ya mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia Shinyanga.
Wadau wakiendelea na Mkutano.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wadau wakiendelea na Mkutano.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa Mkutano.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464