TAASISI YA NANCY FOUNDATION IMETOA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU MANISPAA YA SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
TAASISI ya Nancy Foundation imetoa vifaa vya shule kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu Manispaa ya Shinyanga, ambao awali waliowakomboa kutoka kuishi mitaani na kuwarudisha kwa wazazi wao, vifaa ambavyo watavitumia kwenye masomo yao na kufanya vizuri kitaaluma.
Msaada wa vifaa hivyo vya shule vimetolewa leo Agosti 20, 2023 katika Kanisa na Hosana Pentecost ambalo lipo Kambarage Manispaa ya Shinyanga, Mahali ambapo watoto hao hua wanapata huduma ya kiroho na mafundisho ya watoto siku za Jumamosi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga, akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya shule kwa watoto hao ndani ya Kanisa hilo, amesema kipindi cha utekelezaji wa Programu ya kuwaondoa watoto wa mitaani kwenda kuishi na wazazi wao, walibaini baadhi ya matatizo ambayo huwakabili watoto hao ikiwano na ukosefu wa vifaa vya shule.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga.
Anasema wao kama Taasisi ya Nancy Foundation, licha ya Programu yao kuishi bado wanaendelea kutoa huduma kwa watoto hao, ikiwamo na kuwapeleka kwenye nyumba za Ibada ili wapate mafundisho ya kiroho na kusahau kabisa kurudi kuishi mitaani, pamoja na kuwatimiza mahitaji yao ya shule na kuwalipa chakula na masomo ya ziada.
“Watoto hawa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali licha ya sisi kuwatoa kuishi mitaani na kuwarudisha kwa wazazi wao, tukaona siyo vyema kuwaacha hivi hivi bali tuendeleaa kuwasaidia, na ndiyo maana leo tumewapatia vifaa vya shule, zikiwamo Sare, Soksi, Madaftari, Begi na Kalamu,”amesema Manjerenga.
Watoto wakiwa na vifaa vya shule.
Naye Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila, ameipongeza Taasisi ya Nancy Foundation, kwa kuwakomboa watoto hao kutoka kuishi mitaani na kurudi shule kuendelea na masomo yao ili watimize ndoto zao, na kusema kuwa hiyo neema kubwa kutoka kwa Mungu.
Mchungaji wa Kanisa la Hosana Pentecost Anjelina Kapaya, amesema watoto hao waliwapokea kutoka katika Taasisi hiyo ya Nancy Foundation, na wamekuwa wakiwapatia mafundisho mbalimbali ya kiroho, na sasa wamebadilika na baadhi wamesha anza kuimba Kwaya Kanisa hapo.
Nao baadhi ya watoto hao akiwamo Charles Michael, wameishukuru Taasisi ya Nancy Foundation kwa kuwarudisha tena kwenye upendo na kurudi shule ili kuziishi ndoto zao, na kuahidi kusoma kwa bidii ili kufanya vizuri kitaaluma.
Mmoja wa wazazi wa watoto hao Sophia Samweli, amesema wanafarijika kuona watoto wao wamerejea tena shuleni pamoja na kuendelea kupatiwa vifaa vya shule, na kubainisha kuwa ugumu wa maisha ndiyo uliwafanya kushindwa kuwalea watoto wao, na hatimaye kukimbilia mitaani ili kujitafutia ridhiki.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Lemiflora Nyaraja, amesema katika Programu ya utambuzi wa watoto wa mitaani, walibaini jumla ya watoto 30 na wamewarudisha kwa wazazi wao, kasoro watoto 6 ambao wao walikuwa na hali mbaya zaidi za kimaisha ambao wamewapeleka kwenye kuishi katika Makao ya watoto wilayani Kahama.
Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya Nancy Foundation Neema Mongi akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Vifaa ya Shule kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi Mazingira Magumu Manispaa ya Shinyanga.
Mchungaji wa Kanisa la Hosana Pentecost Church Anjelina Kapaya, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila,akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa Maudhui ya Ubongo Kids Ben Michael akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Lemiflora Nyaraja, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mtoto Charles Michael akitao shukrani.
Mzazi Sophia Samweli akizungumza kwenye hafla hiyo na kutoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine ambao watoto wao wamepewa vifaa vya shule.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya shule kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi mazingira magumu manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya shule kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi mazingira magumu manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya Nancy Foundation Neema Mongi akiandaa vifaa vya shule kwa ajili ya kuvikabidhi kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi katika Mazingira magumu Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga (kulia) akimkabidhi vifaa vya shule Mchungaji wa Kanisa la Hosana Pentecost Church Anjelina Kapaya kwa ajili ya kuvikabidhi kwa baadhi ya watoto ambao wanaishi Mazingira Magumu.
Mchungaji wa Kanisa la Hosana Pentecost Church Anjelina Kapaya, kulia akikabidhi vifaa vya shule kwa mtoto ambaye anaishi Mazingira Magumu.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya shule likiendelea.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya shule likiendelea.
Waumini wa Kanisa la Hosana Pentecost wakishuhudia watoto ambao wanaishi katika Mazingira Magumu wakipewa vifaa vya shule na Taasisi ya Nancy Foundation.

Viongozi wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya shule kwa watoto ambao wanaishi Mazingira Magumu katika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga wakitoa burudani ya nyimbo za kumsifu bwana katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya shule.
Burudani za Nyimbo zikiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa huku watoto wakiwa wameshika vifaa vya shule walivyopewa na Taasisi ya Nancy Foundation.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464