WADAU SHINYANGA WATOA MAONI,MAOMBI MAREKEBISHO BEI MPYA ZA MAJI KUTOKA SHUWASA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WADAU wa Maji Manispaa ya Shinyanga, wametoa maoni yao juu ya Ombi la kurekebisha bei mpya za maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA)Mamlaka hizo za maji zinapaswa kurekebisha bei za maji kila baada ya miaka mitatu, kwa kuwasilisha maombi Ewura pamoja na kushirikisha wananchi kutoa maoni yao.
Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusuph Katopola, akiwasilisha mapendekezo ya bei mpya za maji, amesema licha ya Sheria kuwabana, pia gharama za uzalishaji na usambazaji maji zimeongezeka.
Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusuph Katopola.
Amesema bei za maji ambazo zimekuwa zikitumia niza kuanzia mwaka 2018-2019 ambazo zinatumika hadi sasa, hivyo bei hizo mpya zitatumia kuanzia Septemba 2023 hadi 2026.
Ametaja bei za awali kwamba kwa wateja wa majumbani 5m3 Sh.1,490 na Unit1ilikuwa ni Sh.1,740, Taasisi 2,760, Biashara 2,790, Viwanda 2,850, Vioski 1,500, Viwanda vya Maji na Chupa Sh.3,750.
Mapendekezo ya Bei mpya za maji kwa wateja wa majumbani chini ya 5m3 itakuwa bure, matumizi ya Unit 1 itakuwa Sh. 2,550 kwa mwaka wa fedha (2023/2024), na (2024/2025) Uniti 1 itakuwa Sh.3,190 na (2025/2026) itakuwa Sh.3,630.
Kwa upande wa Taasisi mapendekezo ya bei mpya Unit1 itakuwa Sh.3,270 Mwaka ujao Sh.4,050 na (2026) Sh.4,600, Biashara Sh.5,360 mwaka ujao Sh.5,730, 2026 bei itakuwa Sh.6,510.
Viwanda bei itakuwa Unit 1 Sh.5,400, mwaka ujao Sh. 6010 na (2026)bei itakuwa Sh.6,840, Vioski bei Sh.2,600, (2024/2025) bei Sh.3 200, (2025/2026) bei itakuwa Sh.3,640.
Ametaja pia mapendekezo ya bei mpya za Viwanda vya maji na chupa kuwa mwaka (2023/2024) bei itakuwa Sh.6,110, kwa Unit, (2024/2025) sh.6,240 na (2025/2026) ni Sh.7,100.
Mhandisi Katopola ametaja pia mapendekezo ya huduma za kurejeshewa huduma za maji baada ya kusitishiwa kwamba watendaji wa Majumbani kutoka Sh.10,000 hadi 15,000, Taasisi, Biashara na Viwanda kutoka 20,000 hadi 30,000, Viwanda vya Maji na Chupa kutoka 50,000 hadi Sh. 100,000.
Kwa upande wa Ada za kumwaga Majitaka Magari yenye ujazo chini mita za ujazo 7 kutoka Sh.5,000 hadi Sh.10,000, ziadi ya ujazo Mita 7 kutoka 10,000 hadi 20,000.
Amesema Mamlaka hiyo inatarajia kununia Gari la Majitaka ili kuondoa topetaka kwa wateja na bei itakuwa Sh.11,519, (2024/2025) Sh.12,566 na (2025/2026) Sh.13,708.
"Mapendezo ya marekebisho ya bei hizi mpya yataiwezesha Mamlaka kuwa na uwezo mzuri wa kifedha ili kukidhi gharama za uzalishaji na usambazaji maji, kupanua mtandao wa maji na kufikia wananchi wote," amesema Mhandisi Katopola.
Nao baadhi ya wananchi wakiwasilisha maoni yao juu mapendekezo na maombi ya bei hizo mpya za Maji, baadhi waliunga Mkono ongezeko la bei hizo huku wengine wakipinga na kuomba ziangaliwe upya.
Naye Meneja wa Ewura Kanda ya Ziwa George Mhina, amesema mapendekezo ya bei hizo siyo kwamba ndiyo zimepita, bali watachukua maoni hayo ya wananchi na kwenda kukaa vikao,ndipo watatoa bei halisi ambazo zitatumika kwa kuzingatia vigezo na miongozo ya Sheria.
Meneja wa Ewura Kanda ya Ziwa George Mhina.
Amesema baada ya bei hizo kupitishwa na Ewura, hawatarajii tena kuona Shuwasa wakipeleka maombi ya marekebisho ya bei za maji hadi ndani ya miaka mitatu.
Mgeni Rasmi kwenye Mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ameipongeza Serikali kwa kuweka mambo katika uwazi huku akisisitiza kuendelea kutolewa huduma bora ya maji kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Mwekahazina wa Ewura CCC Mkoa wa Shinyanga Joseph Ndatala akizungumza kwenye Mkutano.
Mwananchi Alley Juma akichangia maoni kwenye Mkutano wa maombi ya Mapendekezo ya bei mpya za maji kutoka Shuwasa.
Mhandisi Silvester Mahole akichangia maoni kwenye Mkutano wa maombi ya Mapendekezo ya bei mpya za maji kutoka Shuwasa.
Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole akichangia maoni kwenye Mkutano huo.
Mwananchi Noela Ilege akitoa maoni kwenye Mkutano huo.
Mwananchi Itendele Bernard akichangia maoni kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakiendelea kutoa maoni.
Wananchi wakiendelea kutoa maoni.
Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Shinyanga Richard Mpongo akitoa maoni kwenye Mkutano huo.
Wadau wa maji wakiwa kwenye Mkutano huo wa kutoa maoni juu ya mapenedezo ya bei mpya za maji kutoka SHUWASA.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464