Polisi wakamata Mawe ya madini ya dhahabu yaliyoibwa Mgodi wa Bulyanhulu
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limekamata vitu mbalimbali vya wizi yakiwamo mawe ya madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 6,753.4 yaliyoibwa katika machimbo ya dhahabu Bulyanhulu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga Janeth Magomi akionyesha Ndoo yenye Mawe waliyosangwa ya Madini ya dhahabu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, ametoa taarifa hiyo leo Agost 23, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari kufuatia misako na doria waliyoifanya kuanzia Julai 26 hadi Agost 22 mwaka huu.
Amesema katika msako huo wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi, yakiwamo mawe yenye madini ya dhahabu yakiwa na thamani ya bilioni 9.2, pia wamekamata Carboni yenye mchanga wenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenye uzito wa kilogram 261, katika maeneo ya Manzese wilayani Kahama.
Kamanda Magoni akionyesha Madumu yenye Carbon mchanga wa madini.
“Madini haya tumeyakamata yakiwa yanatoroshwa ambayo yalikuwa yameibwa katika machimbo ya dhahabu Bulyanhulu, na watuhumiwa tumewakamata wapo rumande,”amesema Magomi.
Aidha, ametaja vitu vingine vya wizi kuwa wamekamata Bunduki aina ya Riffle yenye namba 2/49PF78701 ambayo ilikuwa ikitumika katika shughuli za ulinzi bila kibali, wamekamata pia Bangi yenye uzito wa Kilogram 71, Mafuta ya Dizeli Lita 603 yaliyoibwa katika Mradi wa SGR, Seti moja ya Computer, Pikipiki 3, Tiles Boks 14, Mabomba sita ya chuma.
Kamanda akionyesha Bunduki aina ya Riffle.
Vitu vingine ni Mabati 17, Madumu matatu ya Rangi, Mifuko miwili ya Saruji, Saba ya chokaa, Packet 120 za vipodozi vyenye sumu, huku wakifanikiwa kukamata watuhumiwa 31 ambao wamehusika na matukio hayo ya wizi.
Kamanda akionyesha mafuta ya Dizeli yaliyoibwa katika mradi wa SGR.
Katika hatua nyingine Kamanda alisema wamekamata Magari 3,084 kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani, ikiwamo kutokuwa na leseni, bima, mwendokasi, kuzidisha abiria, huku wakikamata madereva wa pikipiki 229 kwa kutovaa kofia ngumu, kuendesha pikipiki mbovu madereva 64.
Alitaja pia idadi ya kesi ambazo zimepata mafanikio Mahakamani kwa makosa mbalimbali, kwamba kesi hizo zilitolewa hukumu na wahusika kufungwa jela zikiwamo za ubakaji, ulawiti, kutorosha Mwanafunzi, uvunjanji, kusafirisha madawa, kuharibu mali, pamoja na kukiuka masharti ya lesseni ya biashara ambapo mhusika alilipa faini Sh.500,000.
Alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kufuata sheria za nchi na pamoja na kutoa ushirikiano kwa Jeshi kutoa taarifa za uhalifu ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Kamanda akionyesha vitu mbalimbali vya wizi ambavyo wamevikamata.
Kamanda akionyesha madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo wameikamata.
Bangi iliyokamatwa.
Vitu vya wizi vilivyokamatwa.
Vitu vya wizi vilivyokamatwa.
Pikipiki ambazo zimetekelezwa zilizokuwa zikitumika katika uhalifu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464