UWT WAKEMEA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WATOTO


UWT WAKEMEA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WATOTO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) wamekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambavyo vimekuwa vikiendelea hapa nchini dhidi ya watoto wadogo yakiwamo ya ubakaji na ulawiti.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Mary Chatanda amebainisha hay oleo Agost 26,2023 kwenye Mkutano wa hadhara ulioganyika katika viwanja vya Jeshi la Zimamoto Manispaa ya Shinyanga akiwa ameambatana na Makamu wake pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwamo WaNEC na Wabunge wa Vitimaalumu na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, umewataka Wazazi na walezi kujikita katika malezi bora ya watoto wao na siyo kuwaacha wakitanga tanga Mitaani, pamoja na kuwalaza watoto wa kiume chumba kimoja na wageni ambao baadhi wamekuwa wakiwafanyia watoto wa kiume vitendo vya kuwalawiti.

Amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo kwa sasa vimeshamilia na wamekuwa wakifanyiwa na watu wa karibu na kuwataka wazazi, wasiwafiche watu ambao wamekuwa wakifanyika ukatili watoto wao bali wawafichuke ili wachukuliwe hatua kali za kisheria na kukomesha kabisa tatizo la ubakaji na ulawiti watoto.
“Sisi UWT moja ya Ajenda yetu kubwa katika ziara yetu ni kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo na waomba wazazi tuungane kulikemea jambo hili ni baya wafichueni watu ambao hufanyika watoto vitendo vya ubakaji na ulawiti ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria,”amesema Chatanda.

Aidha, amekemea pia tatizo la uchezaji wa vigodoro kwa kuvaa vijora vyepesi huku ndani wakiwa hawana kitu na kujimwagia maji kwamba michezo hiyo haifai sababu imekuwa ni chanzo kubakwa sababu ya kucheza tupu, bali wacheze michezo ya asili yenye kuzingatia maadili ya Mtanzania.
Katika Hatua nyingine amewataka wanawake kuacha kujiingiza kwenye Mikopo kausha damu ambayo imekuwa moja ya chanzo cha kufarakanisha familia zao na kuwarudisha kimaendeleo bali wachangamkie mikopo ya Halmashauri asilimia 10 isiyo na riba ambayo itaanza kutolewa hivi karibuni kwa utaratibu mzuri.

Naye Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari, amewataka Watanzania kumuunga Mkono Rais Samia katika utawake wake ambapo amekuwa akiwaletea fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akitoa Kopyuta 10 kwa baadhi ya Shule ya Sekondari Manispaa ya Shinyanga ili kuendena na utoaji wa elimu kwa njia ya TEHAMA.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wabunge wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia)kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa UWT.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda (kushoto) akikabidhi Kompyuta ambazo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kukabidhi Kompyuta likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Kompyuta likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Kompyuta likiendelea.
Mipira 20 ambayo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi kwa ajili ya kuunga Mkono mashindano ya Mama Samia Cup ambayo yatafanyika Mjini Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464