WATENDAJI MANISPAA YA SHINYANGA WAPONGEZWA KUANDAA TAARIFA YA KUFUNGA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KATIBU Tawala wa wilaya ya Shinyanga Saidi Kitinga, amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kuandaa taarifa nzuri ya kufunga hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha (2022/2023) unaoishia june 30.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Saidi Kitinga.
Amebainisha hayo leo Agosti 29, 2023 wakati akizungumza kwenye kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, cha kupitia taarifa ya hesabu za mwisho zinazoishia june 30, 2023.
Amesema taarifa hiyo imeandaliwa vizuri na kuonyesha kipimo cha utendaji kazi, na imeonyesha watendaji wanafanya kazi kwa ushirikiano, hali ambayo inaonekana kuna uhai wa Halmashauri.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la kufunga hesabu za mwisho.
“Document hii ya taarifa ya hesabu za mwisho jinsi mlivyoiandaa ni kipimo cha utendaji kazi mzuri kwa watendaji wetu wa Halmashauri na wanafanya kazi kwa ushirikiano,”amesema Kitinga.
Aidha, amesisitiza pia suala la ulipaji madeni ambayo inadaiwa halmashauri na wazabuni, umaliziaji miradi viporo, kushughulikia mali chakavu ili kutoongeza thamani ya uchakavu, pamoja na kutoa hamasa ya ukusanyaji mapato kwa watumishi.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la kufunga hesabu za mwisho.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe, amewasihi watendaji pamoja na madiwani waendelee kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi na kusukumua guruduma la maendeleo Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe.
Kaimu Mwekahazina wa Manispaa ya Shinyanga Wallace Kiondo, awali akiwasilisha taarifa hizo za hesabu za mwisho zinazoishia June 30 mwaka huu, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilibaki na jumla ya Sh.bilioni 3.4 ambazo ni fedha zilizokuwa hazijatumika katika ngazi ya Halmashauri na ngazi ya chini ya halmashauri.
Amesema katika fedha hizo Sh. milioni 963.4 ni fedha za bakaa ngazi ya Halmashauri, na Sh.bilioni 2.5 ni fedha za bakaa ngazi ya chini.
Kaimu Mwekahazina wa Manispaa ya Shinyanga Wallace Kiondo.
Amesema bakaa ya fedha za matumizi ya kawaida na Miradi ya maendeleo hadi kufikia june 30 mwaka huu. Kiasi cha Sh.bilioni 1.4 kilibaki kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za matumizi ya kawaida ya miradi ya maendeleo, huku akibainisha kuwa katika mfuko wa Amana halmashauri ilikuwa ni Sh.bilioni 2.1.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Doris Dalio akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.

Baadhi ya wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464