Kishapu wagawa madume ya Ng'ombe aina ya Borani kwa wafugaji.
Na Ofisi ya habari,KISHAPU
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imegawa madume bora ya ng'ombe 38 aina ya borani kwa vikundi vya wafugaji wilayani humo.
Ugawaji wa madume hayo ya Ng'ombe umefanyika leo Agosti 16,2023 katika kijiji cha Mwanashele.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bw, Given Noah amesema ugawaji wa madume hayo bora ya Ng’ombe ni utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa Sekta ya Mifugo.
Amesema kwamba Dume moja la Ng'ombe lina uwezo wa kupanda majike 25 kwa mwaka.
“Mifugo mingi iliyopo hapa Kishapu niya asili na uzalishaji wake wa nyama na maziwa ni ndogo, hivyo madume hayo ya Ng'ombe ambayo tumewapatia utasaidia wafugaji kuwa na mifugo michache ambayo itakuwa na uzalishaji mkubwa wa nyama na maziwa,” amesema Noah
Aidha, amesema kuwa Ng’ombe wa asili huzalisha nyama kilo 80 -120 lakini baada ya kuboreshwa mfugaji anaweza kupata kilo 150 – 200 kwa ng’ombe.
Kwa upande wa maziwa ng’ombe hawa walioboreshwa huwa wanauwezo wa kutoa Maziwa kati ya lita 5 – 10 na hivyo kumfanya mfugaji apate tija zaidi tofauti na mfugaji wa ng’ombe wa asili.
Pia, amewataka Wafugaji hao kuyatunza madume hayo kwa kufuata taratibu zote wanazoelekezwa na wataalam wa mifugo.
''Navitaka vikundi ambavyo vimepatiwa madume haya kuyatumia kwa kushirikiana na wafugaji wengine ili kuhakikisha tija inapatikana kwa wafugaji ndani ya Wilaya ya Kishapu. Amesisitiza
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu. Shija Malisha Ntelezu amesema kwamba Madume haya bora yanatakiwa yatunzwe kwa ajili ya kuongeza tija kwa Wafugaji wa "Ndugu zangu wafugaji sifa namba moja ya Ngo'mbe hawa ni kuwatunza, Ngo'mbe hawa siyo wa kuwachnganya kwenye Ngo'mbe wengi kuwatunza Ngo'mbe hawa ni pamoja na kuwanywesha Maji safi na Salama kwa hiyo ndugu zangu naomba mkawatunze Ngo'ombe hawa kwa kufuaata maeelekezo yote mnayopatiwa na Wataalamu," Amesema Ntelezu
Naye Mwenyekiti wa Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mhe. Richard Dominick, amesema kuwa wataenda kusimamia utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa sekta ya mifugo kwa kuhakikisha Madume hayo yaliyogawiwa kwenye vikundi vya wafugaji yanatunzwa na kutumika ili kuboresha kosaafu na kuleta tija kubwa kwenye sekta ya Uchumi.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Dkt. Sabinus Chaula akiwasilisha taarifa kwa Katibu Tawala amesema kuwa Lengo la Mradi huu unalenga kuboresha kosafu ya mifugo ya asili ili kupata mazao chotala yenye tija kwa wafugaji pamoja na gharama zilizotumika kwenye Mradi wa Madume bora (Boran)
"Ndugu Mgeni Rasmi Lengo la Mradi huu unalenga kuboresha koosafu ya Mifugo ya asili ili kupata mazao chotala nyenye tija kwa wafugaji, Ndugu. Mgeni rasmi gharama ya mradi ni zaidi ya Millioni 121, Mradi huu utasaidia kuboresha kosafu za Mifugo na kupata mifugo yenye uzito mkubwa Ngo'mbe hawa wakifugwa vizuri wanauwezo wakuwa na Uzito wa Kilo 700 mpaka 1000." Amesema Dkt Chaula.
Hata hivyo Dkt. Sabinus amebainisha sifa zilizotumika kuwapata Wafugaji watakaopatiwa madume bora ya Ngo'mbe ni mfugaji mwenye mahusiano bora na wadugaji wenzake, mkazi wa kudumu wa eneo hilo, asiwe na historia ya wizi, mfugaji ambaye anajali mifugo kwa kuwatunza kwa kufuata maaelekezo ya Wataalam kwa kushiriki katika kuwaogesha pamoja na Chanjo.
Diwani wa kata ya Lagana Mhe. Luhende Sana Luhende, amesema kuwa Wanaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dtk. Samia Suluhu Hassan kwa kuona inafaa sana Mradi huu kuwa ndani ya Wilaya ya Kishapu hasa katika kata ya Lagana na ameahidi kushirikiana na wafugaji kuhakikisha Madume hayo yanakuwa salama kwa wakati wote.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Beledi Bw. Dotto Izengo kwa niaba ya Wafugaji wa Wilaya ya Kishapu ameishukuru serikali kupitia Sekta ya Mifugo kwa kuwapelekea wafugaji madume hayo ya ng’ombe yatakayokwenda kuboresha kosaafu na hivyo kuwafanya wazalishe kwa tija na kibiashara.
Aidha Kaimu Katibu Tawala amewakumbusha wafugaji hao kuwa Madume hayo ni Mali ya Halmashauri mpaka pale yatakapo toka maeelekezo mengine.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464