Header Ads Widget

MWENYEKITI WA UWT TAIFA MARY CHATANDA AIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO

MARY CHATANDA AIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Na. Shinyanga RS.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Mary Pius Chatanda ameipongeza Halmasahuri ya Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo huku akiwataka wananchi kuitunza miradi hiyo ili iweze kudumu na kuja kunufaisha na vizazi vijavyo.

Ndg. Mary Chatanda ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga iliyopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, shule ambayo imejengwa awamu ya kwanza kwa fedha za Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya Tzs 4,100,000,000/- (Bilioni nne na milioni mia moja tu) shule hii imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano Agosti 2023.

Kando na pongezi hizo kwa uongozi wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na Manispaa yake Ndg. Mary Chatanda amewataka wananchi wote kuitunza miundombinu hiyo ili iweze iweze kutumika na vizazi vijavyo, huku akiwakata wanafunzi kusoma kwa bidii zaidi ili waweze kufikia malengo yao ukizingatia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekwishatekeleza kila kitu muhimu kwa ajili ya elimu na kilichobakia ni wao tu kusoma kwa bidii.

"Kwa dhati kabisa nawapongeza nyote kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi hii ya maendeleo kwa Wilaya na Manispaa hii ya Shinyanga, miradi hii ni mizuri sana ndugu zangu hakika thamani ya pesa iliyotolewa na Serikali inaonekana wazi kabisa, kazi ni nzuri sana nakupongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, Mstahiki Meya wa Manispaa hii Mhe. Elias Masumbuko, Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze na wataalamu wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine kwa kazi hizi hakika hongereni sana," alisema Ndg. Mary Chatanda.

Shule ya Wasichana Shinyanga imefunguliwa rasmi tarehe 13 Agosti, 2023 na kupokea wanafunzi wa kidato cha tano 70 kwa Tahasusi za masomo ya Sayansi CBG 21, PCB 25, na PCM 24.

Pia Ndg. Mary Chatanda alipata wasaa wa kutembelea na kukagua na Uboreshaji wa Miundombinu Kituo cha Afya Kambarage ambapo Manispaa ya Shinyanga ilipokea Tzs. 500,000,000/- (Milioni mia tano) fedha ambazo zimejenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la wagonjwa wa ndani, jengo la mionzi na njia za watembea kwa miguu.

Kukamilika kwa mradi huu wa Kituo cha Afya Kambarage kutaboresha utoaji wa huduma mbalimbali za afya ikiwamo huduma za uchunguzi, wagonjwa wa nje na wagonjwa watakaolazwa. Aidha uwepo wa Kituo hiki cha afya Kambarage kunakwenda kuwanufaisha wakazi wa Kata hii ya Kambarage pamoja na maeneo jirani yanayozunguuka eneo hili.

Post a Comment

0 Comments