WAJUMBE WA KAMATI EWURA CCC MKOA WA SHINYANGA WARIDHISHWA NA SHUWASA KUTOA HUDUMA BORA YA MAJI KWA WANANCHI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WAJUMBE wa Kamati ya Mkoa ya Watumiaji Maji na Nishati (Ewura CCC) mkoani Shinyanga,wametembelea miradi ya maji ambayo imetekelezwa na Shuwasa, na kujionea namna wanavyotoa huduma bora ya maji kwa wananchi.
Wamefanya ziara hiyo leo Agosti 17,2023 kwa kutembelea baadhi ya Miradi ya Maji katika Mji wa Didia na Tinde,na kuona namna huduma za maji zinavyotolewa kwa wananchi.
Mwekahazina wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC Mkoa wa Shinyanga Joseph Ndatala (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusuph Katopola kwenye Tangi la Mradi wa Maji Didia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga Kudely Sokoine, amesema katika ziara hiyo wameona namna Shuwasa wanavyowajibika katika kutekeleza miradi ya maji kwa kiwango bora na kutoa huduma stahiki ya maji kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga Kudely Sokoine.
"Katika ziara hii tumeona uwajibikaji na miradi ya maji imejengwa kwa kiwango bora na thamani ya fedha imeoneka, na huduma bora za maji zinatolewa kwa wananchi isapavyo tunawapongeza sana Shuwasa," amesema Sokoine.
Aidha, amewataka pia Wananchi kuendelea kuitunza miundombinu ya miradi hiyo ya maji, pamoja na kulipa Bili za Maji kwa wakati, ili Mamlaka hiyo ipate pesa na kuendelea kupanua mtandao wa kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Naye Katibu wa Kamati hiyo Zezema Shilungushela, ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kuzielekeza kwenye utekelezaji wa miradi ya maji, ambayo imewaondolea adha wananchi ya ukosefu wa Majisafi na salama.
Katibu wa Kamati Mkoa Ewura CCC Mkoa wa Shinyanga Zezema Shilungushela
Mwekahazina wa Kamati hiyo Joseph Ndatala, amewasihi Shuwasa kuendelea na utoaji wa huduma bora ya maji kwa wananchi, pamoja na k kutatua changamoto kwa wakati ikiwamo upasukaji wa mabomba.
Nao baadhi ya wananchi akiwamo Asha Hamadi mkazi wa mji wa Didia, amesema kwa sasa hawana shida tena ya Majisafi na salama kama hapo zamani,na kuishukuru Shuwasa kwa utekelezaji wa miradi hiyo ya maji.
Mwananchi Asha Hamadi.
Mwananchi Mwingine Paulo Bwire, amesema zamani walikuwa wakinunua maji dumu moja Sh.500, lakini sasa hivi hawana tena Shida ya maji na baadhi ya wananchi wameshavuta maji majumbani mwao.
Mwananchi Paulo Bwire.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amesema awali walikuwa wakitekeleza miradi ya maji Manispaa ya Shinyanga pekee, lakini Serikali ikawaongezea wigo kutoa huduma ya maji katika mji wa Tinde, Didia na Iselamagazi wilayani Shinyanga.
Amesema ana mshukuru Rais Samia kupitia Wizara ya Maji, kwa kuendelea kutoa fedha na kutekelezwa miradi ya maji, na kwamba katika Mji wa Didia kimetolewa tena kiasi cha fedha Sh.milioni 700 kwa ajili ya kuongeza mtandao wa maji, kutokana na kuwapo kwa mradi wa Reli ya kisasa SGR.
Aidha, amesema Mamlaka hiyo itaendelea kutoa huduma bora ya maji kwa wananchi, na wale ambao bado hajawafikiwa na huduma hiyo katika maeneo ambayo wanatekeleza miradi, wote watafikiwa na maji hayo kutoka Ziwa Victoria.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)Mhandisi Yusuph Katopola akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maji.
Mwananchi Daud Elikana mkazi wa Didia wilayani Shinyanga akizungumza namna wanavyonufaika na mradi wa maji ya Ziwa Victoria.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga wakiwa katika Tangi la mradi wa maji Didia wilayani Shinyanga.
Mwekahazina wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC Mkoa wa Shinyanga Joseph Ndatala (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusph Katopola kwenye Tangi la Mradi wa Maji Didia.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga wakiwa katika Tangi la mradi wa maji Didia wilayani Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga wakiwa katika Tangi la mradi wa maji Didia wilayani Shinyanga, kushoto ni Mkurugenzi wa (SHUWASA) Mhandisi Yusup Katopola.
Kaimu Mkurugenzi wa usambazaji Maji na usafi wa Mazingira kutoka SHUWASA Mhandisi Uswege Mussa akitoa maelezo namna wanavyotekeleza miradi ya maji na kutoa huduma kwa wananchi
Baadhi ya wananchi wa Didia wakiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ewura mkoani Shinyanga kwenye Tangi la Maji Didia.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa ya Ewura CCC mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Tangi la Mradi wa Maji Ziwa Victoria lililopo kijiji cha Buchama.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja katika Tangi la Mradi wa Maji Ziwa Victoria Tinde, lililopo kijiji cha Buchama.
Katibu wa Kamati ya Mkoa Ewura CCC mkoani Shinyanga Zezema Shilungushela (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Afisa Uhusiano SHUWASA Nsianel Gerald kwenye jiwe la msingi la mradi wa maji Ziwa Victoria lililowekwa na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango Januari 19 mwaka huu.
Wajumbe wa Kamati ya Mkoa Eruwa CCC Mkoa wa Shinyanga katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa SHUWASA na Afisa Mahusiano.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464