VIGOGO WAJIFUNGIA KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA BILIONI 9 ZAPITISHWA KUANZA UTEKELEZAJI


Vigogo wastaafu wajifungia kujadili mchakato wa Katiba mpya

Waziri wa Katiba na Sheria, 

Tayari Bunge limepitisha bajeti ya Sh9 bilioni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mchakato wa Katiba mpya. Hata hivyo, haijulikani ni mchakato huo utafikia tamati na nchi kupata Katiba mpya.

Dar es Salaam. Wizara ya Katiba na Sheria, imewakutanisha pamoja mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wastaafu na waliopo madarakani katika kikao chenye lengo la maoni yao kuhusu mchakato kupata Katiba mpya.

Waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika leo Agosti 28, 2023 jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akiwa kama Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, Joseph Warioba na Mizengo Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora.

Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464