Rais Samia ataka unafuu mbolea ya ruzuku
Rais Samia aagiza viongozi wa Wizara za Kilimo pamoja na Wizara ya Fedha, kukaa pamoja ili kuangalia gharama za kupelekea mbolea ya ruzuku kwa bei nafuu kwa wakulima wa maeneo mbalimbali.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemwagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kukaa na Wizara ya Fedha ili kuangalia gharama za usambazaji wa mbolea ya ruzuku kwa lengo la kuleta unafuu kwa wakulima.
Rais Samia ametoa agizo hilo, leo Jumatano Agosti 8, 2023 katika kilele cha maonyesho ya Wakulima, Nanenane yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Maonyesho ya mwaka huu, yamebeba kauli mbiu ya ‘vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula’. Ambapo Rais Samia amesema kauli mbiu hiyo inalenga kutambua mchango wa vijana na wanawake katika kilimo, mifugo na uvuvi.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464