Na Mwandishi wetu - Shinyanga Press blog
Mahafali ya 11 ya chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga yamefanyika ambapo jumla ya wahitimu 253 wametunukiwa stashahada ya kozi mbalimbali za Afya ya binadamu na ufundi.
Mahafali hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa mkombozi uliopo chuoni hapo ambapo mgeni rasmi ni Askofu Mkuu wa Africa Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Mussa Masanja Magwesela.
Kabla ya wahitimu kuingia ukumbini, mahafali hayo yalitanguliwa na zoezi la uzinduzi wa Jengo jipya lenye madarasa mawili,Ofisi na ukumbi wa mikutano pamoja na ukaguzi wa miundo mbinu ya majengo ya chuo.
Akihutubia kusanyiko la mahafali hayo Askofu Magwesela amewataka wahitimu kuwa na ujasiri wa kwenda kulitumikia Taifa pamoja na kutoa Huduma stahiki kama walivyofundishwa na waalimu wao darasani.
Awali Mkuu wa Chuo hicho Mwl. Paschal Shiluka alizungumzia changamoto na mafanikio ya chuo hicho zikiwa ni pamoja na kutokuwepo Kwa mgahawa wa Chuo ambao ungewasaidia wanafunzi kupata chakula cha uhakika muda wowote.
Kwa upande wa mafanikio amesema chuo kimefanikiwa kusajili kozi za Physiotherapy na Radiology zitakazoanza mwezi September mwaka huu pamoja na kuendelea na mchakato wa kukifanya chuo hicho kuwa chuo kikuu.
Akijibu changamoto hizo askofu Magwesela amesema changamoto ya mgahawa hiyo wataitatua haraka iwezekanavyo,pia ametoa pongezi Kwa uogozi wa Chuo kupambania taaluma hadi kufikia kupata vigezo vya kusajili kozi mpya za Physiotherapy na Radiology.
Aidha wahitimu kutoka kozi ya Uuguzi na ukunga ni 36,Utabibu 81,Maabara ya binadamu 40,Famasia 88 na kozi za ufundi ikiwemo ya Maabara za viwanda ni 08 ambao wanafikisha jumla ya wahitimu 253 kutunukiwa stashahada.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464