Sheikhe wa wilaya ya Kahama Alhaji Omary Damka akitoa Elimu kwa vijana namna ya kusaidia jamii
Na Kareny Masasy,
Kahama
JUMUIYA ya vijana wa dini ya kiislamu Bakwata (JUVIKIBA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha mwaka wa kiislamu ulioenda sambamba na uchangiaji wa damu salama lengo kuokoa wajawazito na watoto.
Wakiadhimisha jana tarehe 6/08/2023 katika msikiti wa ijumaa wilayani Kahama ambapo mwenyekiti wa jumuiya ya vijana Hassan Haruna amesema jumuiya hiyo ina vijana 218 na wamebadilika sasa na wamekuwa wakitoa elimu ya kupinga madawa ya kulevya,ndoa za jinsia moja kwa vijana.
Haruna amesema wao vijana wameona kuwasaidia wanawake katika mradi wao wa ujenzi wa ukumbi wenye kuhitaji sh Millioni 48 kukamilika ambapo msingi umetumia sh Millioni 27 na mpaka msingi kukamilika bado zinahitajika sh Millioni 6.
Mjumbe wa baraza la Masheikhe mkoa wa Shinyanga Ibrahim Manyangali amesema uhitaji wa damu lazima itolewe kwa mtu na mungu ndiyo alivyoumba na damu inatengenezwa kwenye tishu nani seli ndiyo inayozalishawa kwenye mwili pia chakula cha binadamu lazima kipitie kwenye tishu ndiyo maana imeshindikana damu kutengenezwa.
Sheikhe wa wilaya ya Kahama Alhaji Omary Damka amewapongeza vijana kuja na mawazo mazuri waendelee kupiga vita madawa ya kuelevya na ndoa za jinsia moja pia kumsaidia Rais kwani anaweza na anaongoza vizuri nchi hii.
Sheikhe kutoka mkoa wa Mwanza Hassan Kabeka amesema uislamu ulikuwepo tangu zamani na vitabu vimeandika uislamu lazima uwe na moyo wa kutoa kuisaidia jamii jambo la kutoa damu kwa vijana ni ishara ya upendo kwa watu wote.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Azan Said maarufu Mufti amesema mwaka huu wa kiislamu ambao ni 1445 amewapongeza vijana nakuwataka vijana wawe karibu na masheikhe na wazazi ili waweze kusaidiwa na kufanikiwa na utoaji wa damu kwa vijana wahamasishane kwani 42 ni wachache kwa takwimu iliyopo.
“Nitatoa sh Millioni sita kukamilisha msingi na sh Millioni moja kwaajili ya kufungua akaunti kwa wanawake ninawaomba mfanye bidii katika biashara zenu na kuunda vikundi ili viweze kuwasaidia na kujisimamia”amesema Azan.
Mratibu wa
damu salama kutoka hospitali ya manispaa Kahama Noel Malaki amesema vijana 42
wamejitokeza kuchangia damu salama kwa siku ya leo anatoa wito watu wengine
wajitokeze kwa mahitaji ni makubwa na kundi kubwa lenye uhitaji zaidi ni
wajawazito,watoto na wanaopata ajali.
Sheikhe kutoka mkoani Mwanza Hassan Kabeka akiwa katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kiislamu baada ya kukaribishwa na vijana wa dini hiyo wilayani Kahama.
Mama wa akichangia damu salama kwaajili ya kuokoa maisha ya wajawazito na watoto katika maadhimisho ya mwaka mpya
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika hatua ya kujiandaa kutoa damu salama.
Baadhi ya wanawake wa dini ya kiislamu wakiwa msikitini wakisikiliza elimu kutoka kwa viongozi wao wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Mgeni rasm Azan Said maarufu Mufti katika maadhmisho ya mwaka mpya wa kiislamu yaliyoandaliwa na jumuiya ya vijana wa dini hiyo wilayani Kahama.
Viongozi wa dini wakiwa meza kuu