Kishapu yapongezwa usimamizi miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi
Na Ofisi ya Habari, KISHAPU
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dr. Sweetbert Zakaria Mkama ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa usimamizi Mzuri wa Miradi ya kuhimili Mabadiliko ya Tabia Nchi vijijini (EBBAR) inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.
Naibu Mkama Ameyasema hayo Leo Agosti 12, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kishapu yenye lengo la kukagua miradi ya (EBBAR) inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais
"Ndugu zangu WanaKishapu naomba niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa Miradi miradi Mingi imekamilika nikiangalia Malambo, Jengo la kunenepeshea Mifugo lipo tayari Shughuli ndogondogo zilibaki tutazikamilisha ikiwemo ujenzi wa kibanda cha Mlinzi kwenye mradi wa kunenepeshea Mifugo kijiji cha Muguda, Pamoja na ukamilishaji wa Mabanda ya Kufugia Ngo'mbe.
"pia naomba ndugu zangu wananchi niwaambie, Miradi hii siyo ya Ofisi ya Makamu wa Rais ni Miradi yenu tuitunze sana na Miradi hii ni kwaajili ya Utunzaji wa Mazingira katika Wilaya yenu." Amesema Dkt. Mkama
Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo, ameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt, Samia suluhu Hassan kwa kutekeleza Miradi ya (EBBAR) kwa Vitendo ndani ya Wilaya ya Kishapu kwa Sababu Miradi hii imekuwa msaada Mkubwa sana kwa Wananchi wa Kishapu hususani kwa Kata ya Kiloleli na Lagana
"Nitumie furusa hii kumshukuru Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kweli Rais wetu amekuwa Rais wa Vitendo kwa sababu mpango huu wa (EBBAR) umekwenda kuwa mkombozi mkubwa sana katika Wilaya yetu ya Kishapu hususani Kata ya Kiloleli na Lagana,
" Tumeona Miradi Ya Malambo Muguda, kiloleli na Beledi pia Miradi ya Unenepeshaji wa Mifugo, Mradi wa ushonaji wa Viatu vya Ngozi pia Naibu katibu Mkuu tumeshuhudia Madume Bora ya Ngo'mbe aina ya Borani ambayo yanakwenda kuinua ufugaji wa Kisasa kwenye Wilaya yetu." amesema Butondo.
Pia, Mhe. Butondo Ameahidi kuendelea kutoa Ushirikiano Mkubwa kwa kuitunza Miradi yote ambayo inaletwa Serikali kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi.
Katika ziara yake Naibu Katibu Mkuu Dkt. Mkama alikagua kiwanda kidogo cha kunenepeshea Mifugo, Malambo Matatu ya Maji kwa kata ya Kiloleli na Lagana Pamoja na Mradi wa Madume ya Ngo'mbe aina ya Borani na kuagiza ipandwe Miti kwenye Maeneo ya Miradi hasa Malambo kwaajili ya Utunzaji wa Mazingira kama sera inavyotaka.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Dkt. Sabinus Chaula ameahidi kutekeleza na kuyafanyia kazi Maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu kwa Maslahi Mapana ya Halmashauri ya Kishapu.
Aidha Dkt Mkama Amewataka wasimamizi wote wa Miradi hii kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia wajibu wake ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinazaa matunda kwa wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464