Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakipitia taarifa zilizowasilishwa kwenye kwenye kikao cha baraza.
Na Kareny Masasy,
Shinyanga
MADIWANI wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wameomba kuwepo kwa watendaji mitaa au vijiji kwani kukosekana kwao kumeonekana kukwamisha baadhi shughuli za kimaendeleo na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi wa maeneo husika.
Madiwani hao kwa nyakati tofauti wameongea kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani la robo ya nne ya mwaka wakati wakiwasilisha taarifa za kata leo tarehe 9/08/2023.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Msabila Malale,diwani wa kata ya Kolandoto Musa na diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya wamesema baadhi ya mitaa kwenye kata zao hazina watendaji wa mitaa.
Diwani Sheila Mshandete wakati akiwasilisha taarifa ya kata ya Ndembezi amesema mitaa mitatu haina watenda huku diwani wa kata ya Kizumbi akieleza kijiji kimoja hakina mtendaji na kata ya chamaguha mitaa miwili haina watendaji.
Diwani Malale amesema bado kuna changamoto kwenye shule ya sekondari Uzogore kuna matundu ya vyoo manne na hakuna choo cha walimu.
Malale amesema hakuna pia watendaji wa vijiji vitatu ambavyo ni Mwagala,Bugweto A na kijiji cha Ibadakuli hivyo waliiomba manispaa kufanya utaratibu wa kuwapatia watendaji hao.
Diwani wa kata ya Mwamalili James Matinde amesema vijiji vitatu havina watendaji nakueleza changamoto ya kata hiyo kukosa nishati ya umeme na maji pamoja na uhaba wa walimu shule za msingi na sekondari.
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema kweli madiwani kwenye maeneo yao wanakero nyingi na shule zote zina uhaba wa walimu ikiwemo uwiano wa walimu wa kike na wakiume shuleni hauko sawa.
“Suala la kata ya Mwamalili kukosa nishati ya umeme hilo walifanya ziara na Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi nakuwashirikisha Tanesco na mkandarasi aliahidi ndani ya wiki hii ataanza kazi ya kuweka umeme wa REA.”amesema Masumbuko.
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Said Kitinga amesema matundu ya vyoo shuleni ni muhimu kuwepo kwani kulikuwa na kampeni ya nyumba ni choo hivyo walimu nao ni watumishi wanatakiwa wadhamniniwe kupata mahari pazuri pa kufundishia.
Kaimu
mkurugenzi wa Manispaa ambaye ni
mwanasheria Doris Dalia amesema juhudi za serikali zinafanyika ili kuweza
kupata watumishi hao na shule kukosa
vyoo hilo linashughulikiwa kwa haraka lakini liliwekwa kwenye mpango wa bajeti wa
mwaka wa fedha huu na jamii inatakiwa ianze kuchangia ujenzi huo.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakipitia taarifa zinazowasilishwa leo
Madiwani wakisikiliza kikao cha baraza manispaa ya Shinyanga