Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye baraza.
Na Kareny Masasy,Ushetu
MADIWANI wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameomba changamoto za nishati ya umeme,maji na barabara zitatuliwe kwani mara kwa mara wamekuwa wakiongea kwenye vikao.
Madiwani hao wakiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani leo tarehe 23/04/2023 katika kikao cha robo ya nne ya mwaka diwani viti maalum Felister Kabasi akizungumzia changamoto ya barabara itokayo kwenye kata ya Sabasabini na kuelekea Mpunze imekuwa haipitiki kirahisi mashimo ni mengi.
Diwani Kabasi amesema ipo changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme kwani wameona nguzo zimesimikwa siku nyingi lakini hakuna kinachoendelea huku diwani wa kata ya Chona Mabala Mlolwa akieleza kasi ya mkandarasi aliyepewa tenda ni ndogo hivyo mkurugenzi anao uwezo wa kuongea na meneja wa shirika la umeme (Tanesco) kujua changamoto ni nini.
Msafiri Maganga amesema changamoto kubwa ya uhitaji wa maji safi na salama ambapo kata ya sabasabini ,igwamanoni na Mpunze yaliwekwa mabomba lakini mara kwa mara yamekuwa yakipasuka nakuleta uhaba wa maji kwa wananchi.
Diwani Msafiri amesema shule ya sekondari Mpunze inachangamoto ya uhaba wa walimu wa kike ikiwa wanafunzi waliopo wanahitaji kuwepo walimu hao kiutaratibu unaofahamika.
Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,afya na maji Kulwa Shoto akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo amesema kuna visima vinne virefu vinavyotoa maji ambapo Bugomela.Busenda,Chona na Ubagwe na vinasaidia kuwasambazia maji hata kwenye vijiji vingine.
“Kata ya Sabasabini ina mradi wa maji wa kisima kirefu unapeleka kwenye kijiji cha Iponyanholo lakini waliomba wakala wa maji safi na Mazingira vijijini (Ruwasa) wapanue wigo na maeneo mengine wapate maji safi”amesema Shoto.
Aidha akizungumzia uhaba wa walimu wa kike Shoto amesema hata shule ya Sekondari Kinamapula inauhitaji wa walimu wa kike ambapo serikali ilitoa ajira ya walimu kumi wa kike ambao walipokelewa na kupelekwa maeneo tofauti tofauti ila uhitaji bado ni mkubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Hadija Mohamed amesema kweli kuna upungufu wa walimu wa kike hivyo baraza lililopita liliagiza halmashauri iandike barua kuomba Tamisemi na agizo hilo limetekelezwa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Uhsetu Gagi Lala akiongoza kikao cha baraza la madiwani
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Hadija Mohamedi akisoma ajenda za kikao cha baraza la madiwani.
Wataalamu wa halmashauri ya Ushetu wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464