MADIWANI SHINYANGA WAOMBA MTANDAO WA MAJI, HUKU MANISPAA IKIIBUKA NA TUZO YA USAFI WA MAZINGIRA



Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko Kombe la ushindi wa masuala ya usafi wa mazingira

Suzy Luhende,Shinyanga Press 

Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wameiomba Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Shuwasa) kuwatengenezea mtandao wa Maji wakazi wa Kata za Mwamalili, Chibe na Kizumbi kwani maeneo hayo baadhi ya wakazi hawajapata maji safi na salama kutoka ziwa Victoria.

Wameyasema hayo leo kwenye kikao cha balaza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Shinyanga ambapo walihoji taarifa mbalimbali zilizotolewa ikiwemo taarifa ya maji safi na salama katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2022,2023.

Madiwani hao ambao ni diwani wa kata ya Mwamalili James Matinde Furushi, diwani wa kata ya Chibe John Kisandu na diwani wa Kata ya Kizumbi Ruben Kitinya wakiuliza Mamlaka ya Maji Wilaya ya Shinyanga kuwa nilini Maji yatapelekwa kwa wananchi.

Akijibu maswali hayo Kaimu Mkurugenzi Usabazaji Maji na Usimamizi wa Usafi mhandisi Uswege Musa amesema baadhi ya miradi inahitaji bajeti kubwa na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu ili wapate fedha za bajeti kwaajili ya kukamilisha shughuli hizo huku wengine akiwaahidi kutafuta mbadara ili kutatua changamoto hizo.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amewataka Shuwasa na Kashuwasa kuwasiliana na Mkurugenzi katika utekelezaji wa miradi ya maji ili awezekuwafahamisha maeneo ambayo yanayohitaji huduma ya maji.

Aidha Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema manispaa ya Shinyanga imeibuka kuwa mshindi wa kwanza katika masuala ya usafi wa mazingira kimkoa ambapo imepata tuzo na zawadi mbalimbali kutoka katika ofisi ya Mkoa na shirika la kimataifa SNV.

"Mkoa wa Shinyanga una manispaa mbili manispaa ya Kahama na Manispaa yetu ambayo imepata heshima kubwa imepata tuzo na zawadi mbalimbali kwa kuwa mshindi wa kwanza kimkoa kwenye masuala ya usafi wa mazingira tumepewa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye masuala ya usafi wa mazingira hivyo nawapongeza sana viongozi mbalimbali wa manispaa kwa kusimamia suala la usafi niwaombe tuendelee kusimamia ili manispaa yetu iendelee kuwa safi"amesema Kagunze.

Pia manispaa ya Shinyanga imekuwa ya kwanza katika masuala ya lishe ambapo imepata alama ya kijani ikifuatiwa na halmashauri ya Kahama mji ambayo nayo imepata alama ya kijani" hivyo nieaombe tuendelee kutekeleza majukumu yetu ili tuendelee kufanya vizuri zaidi hata kwenye miradi mbalimbali
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko tuzo iliyopata manispaa baada ya kushinda masuala ya usafi wa mazingira ya manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko cheti cha usafi wa mazingira baada ya kupata ushindi
Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akionyesha kombe lililotolewa baada ya manispaa hiyo kupata ushindi wa usafi wa mazingira

Sheila Mshandete akiwa ameshikilia kombe baada ya manispaa kupata ushindi
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha baraza la manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akizungumza kwenye baraza la madiwani
Diwani wa manispaa ya Shinyanga James Matinde Furushi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani

Diwani wa kata ya Ibadakuli Msabila Malale akizungumza kwenye baraza la madiwani

Diwani wa kata ya Kizumbe Reuben Kitinya akizungumza kwenye kikao cha madiwani

Diwani viti maalumu Mariam Nyangaka akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani viti maalumu Mariam Nyangaka akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akizungumza kwenye baraza la madiwani
Madiwani wa manispaa wakiendelea kufuatilia makabrasha kwenye kikao
Madiwani wa manispaa wakiendelea kufuatilia makabrasha kwenye kikao
Madiwani wa manispaa wakiendelea kufuatilia makabrasha kwenye kikao
Diwani wa kata ya Ibinzamata Ezekiel Kisabo akifafanua jambo kwenye kikao cha baraza
Madiwani wa manispaa wakiendelea kufuatilia makabrasha kwenye kikao
Madiwani wa manispaa wakiendelea kufuatilia makabrasha kwenye kikao
Viongozi wa chama katika manispaa ya Shinyanga wakiendelea kufuatilia taarifa mbalimbali zaaendeleo katika manispas ya Shinyanga

Alpha Mangula akizungumza kwa niaba ya Leons Mwenda afisa mazingira wa mradi wa kuboresha miliki za ardhi

Dorice Dario mwanasheria Manispaa ya Shinyanga akifafanua jambo la kisheria

Afisa mipango wa manispaa ya Shinyanga Salumu Peter Ndongo akifafanua jambo kwenye baraza la madiwani manispaa


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464