Baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari Mwawaza na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Salome pamoja na mwanafunzi aliyeshinda Chemsha bongo na Salome Makamba akiwa amebeba zawadi zake.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza na wanafunzi wakati wakukabidhi zawadi za Chemsha bongo
Na Shinyanga Press Club Blog
Wanafunzi wa shule za sekondari Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuzingatia masomo ili watimize ndoto zao na kujiepusha na makundi maovu ambayo yanaweza kuwa kikwazo kufikia malengo yao.
Hayo yameelezwa leo Agost 21/2023 na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba wakati akitoa zawadi kwa washindi wa chemsha bongo na Salome Makamba kupitia Radio Faraja baada ya kutembekea shule ya Sekondari Mwawaza, Uhuru na Ngokolo.
Makamba amewataka wanafunzi kuwa wabunifu na kuzingatia wanayofundishwa na walimu wao ili waweze kufikia malengo yao na kujiepusha na makundi ama vitendo ambavyo vinaweza kuharibu ndoto zao .
Amesema chemsha bongo hiyo inashirikisha makundi yote wakiwemo wanawake kupitia vikundi, watu wenye ulemavu,vijana, wanafunzi shule za msingi na Sekondari,wanamichezo na watu binafsi.
Amesema washindi hao wa Chemsha bongo na Salome makamba awamu ya kwanza, wamepatikana baada ya kujibu kwa usahihi maswali yaliyokuwa yakiulizwa kupitia vipindi mbalimbali vya Redio Faraja ambapo waliofanikiwa kujibu maswali vizuri wamekabidhiwa zawadi zao.
Amesema lengo ni kuibua vipaji na kuwapa wananchi msukumo wa kutafuta taarifa kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kufuatilia na kujua mipango ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Kwa upande wake mratibu wa chemsha bongo na Salome Makamba kupitia Radio Faraja Simeo Makoba amesema chemsha bongo imehusisha watu wenye ulemavu,wazee, vijana, wanawake na wanafunzi, ambao leo wamekabidhiwa zawadi.
Katika zawadi hizo vikundi vilivyoshinda kikiwemo kikundi cha Papo kwa papo na kikundi cha walemavu wasioona Kambarage wamepatiwa zawadi ya fedha taslimu Sh laki 300,000 kila kikundi.
Zawadi zingine zilizokabidhiwa kwa washindi ni majiko ya gesi, Tisheti, Jezi na Mpira wa miguu kwa timu za mpira pamoja na vifaa vya shule kwa wanafunzi walioshiriki chemsha bongo na kushinda kutoka shule tatu za sekondari na taulo za kike.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Ngokolo sekondari Jasmin Mabruck akipokea zawadi baada ya kushinda chemsha bongo na Salome Makamba akiwa ni binti peke yake ambapo pia amepewa zawadi ya makaunta book 7 na taulo za kike
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ngokolo
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mwawaza wakiwa na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba baada ya kutembelea shule hiyo kukabidhi zawadi kwa mshindi wa chemsha bongo na Salome Makamba kupitia Radio Faraja
kwa washindi wa Chemsha bongo
Wanafunzi wa shule ya sekondari UhuruMratibu wa chemsha bongo na Salome Makamba kupitia Radio Faraja Simeo Makoba akitoa neno kwa wanafunzi
Mkuu wa shule ya sekondari Uhuru Victoria Nakiliaumi akizungumza na wanafunzi baada ya mwanafunzi wake kutangazwa kuwa mshindi wa chemsha bongo na Salome MakambaMwanafunzi Riziki Benedict wa Uhuru sekondari akipokea zawadi zake Mshindi wa jiko la gasi kupitia chemsha bongo na Salome MakambaMshindi wa jiko la gasi Vicent Ndyamkama akipokea zawadi yake
Washindi timu ya mpira wakikabidhiwa zawadi
Washindi timu ya mpira wa miguu wakikabidhiwa zawadi
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu akipokea zawadi ya Sh laki 300,000 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza na wanafunzi wakati wakukabidhi zawadi kwa washindi wa Chemsha bongo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464