MIUNDOMBINU BORA YA ELIMU SHULE YA SEKONDARI MWAKATA YAIMARISHWA KUONGEZA WATAALAM WA SAYANSI

Mkuu wa shule ya sekondari Mwakata akitoa maelezo namna ambavyo maabara hiyo itasaidia kuwa na wataalam wengi wa sayansi.

Matukio kwenye picha Ziara ya *Makamu mwenyekiti wa UWT MNEC. Zainab Shomari* mapema leo Agosti 28.2023 akiwa wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga  ametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Maabara ya masomo ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwakata iliyopo Kata ya Mwakata halmashauri ya  Msalala Wilaya ya Kahama.

Ujenzi huo umegharimu jumla ya shilingi  milioni 70,299,000 ambapo uwepo wa maabara shuleni hapo umetajwa kuamsha hari na morari kwa wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi,kuongeza ufaulu na umewawezesha walimu shuleni hapo kutotumia nguvu kubwa katika ufundishaji kwa vitendo.

Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akiwa katika shule ya Sekondari Mwakata ambapo ametembelea jengo la maabara na kuona namna ambavyo wanafunzi wanapata utaalamu kupitia masomo ya sayansi.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akiwa na viongozi wengine baada ya kukagua jengo la maabara ya sayansi
  
Wakazi wa Mwakata wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti UWT Taifa  baada ya kukagua jengo la maabara ya sayansi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464