Mwenge wa Uhuru ulipowasili halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga na kuona,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika Miradi ya Maendeleo.
Kareny Masasy,
Msalala
MWENGE wa Uhuru umefika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani
Shinyanga nakuzindua miradi mitano ya Maendeleo ikiwemo ya Elimu na Afya na Maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Abdalla Shaib Kaim LEO tarehe 1/08/2023 ameweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya Elimu kwa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum na kituo cha Afya kilichopo kijiji cha Busungo kata ya Segese.
Kaim ameweka
jiwe la Msingi kituo cha Afya hicho ambacho kimejengwa kwa mapato ya ndani
zaidi ya sh Millioni 400 kwa lengo la kuwaondolea wananchi kutembea umbali
mrefu.
Kiongozi
huyo amekagua na kuona shughuli za
kikundi cha vijana mafundi kwa kujionea thamani
zilizopo baada ya kukopa Mkopo wa asilimia 10 kwenye halmashauri.
Kaim amekagua pia eneo lililotengwa kwaajili ya uhifadhi wa
mazingira na upandaji wa miti kwenye Zahanati ya Masabi kata ya Mega.
Kutokana na
Salamu mbalimbali zinazotolewa na
viongozi kwenda kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kiongozi huyo wa Mwenge kitaifa ameahidi
kuzifikisha salamu hizo ikiwemo pongezi kwa kuleta fedha za kutekeleza Miradi
ya Maendeleo.
Mbunge wa
viti Maalum Santiel Chilumba amesema jitihada zinazofanywa na serikali ni
kutekeleza sera ya afya ya mwaka 2007
kuwa wananchi wasitembee umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mbunge wa jimbo la Msalala Idd Kassim amesema serikali ya awamu ya sita imeleta fedha nyingi kwenye halmashauri hiyo kwaajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo hivyo anastahili kupongezwa.k
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464