Madarasa ya shule ya msingi nguzombili Kata ya Maganzo ambayo yamejengwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Na mwandishi wetu
Makamu Mwenyekiti wa UWT MNEC. Zainab Shomari ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Nguzombili iliyopo Kata ya Maganzo wilayani Kishapu iliyopokea jumla ya shilingi Milioni 561,100,000.
Akizungumza na wanafunzi wa Shule jirani ya msingi Jitegemee na wananchi wanaoshiriki shughuli za ujenzi wa shule hiyo mpya MNEC. Zainab Shomari ambaye yupo kwenye Ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga na viongozi wa UWT Taifa,amefafanua kuwa viongozi wa CCM wakiwemo viongozi wa jumuiya ya wanawake wanatembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu inayotekelezwa na Serikali ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM ya 2020-2025.
“Serikali hii ni ya CCM,miradi hii yote ya maendeleo sisi ndio wasimamizi na watekelezaji.Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dk. Samia ni mdau mkubwa wa elimu ndio maana mnaona amewaletea Shule hii kubwa na ya kisasa,Rai yangu wanafunzi msome kwa bidii”Amesema MNEC. Zainab Shomari.
Mradi huo wa Shule mpya ya Msingi Nguzombili una madarasa 14 ya msingi,madarasa 2 ya awali ya mfano,matundu 16 ya choo kwa shule ya msingi,matundu 6 ya choo kwa shule ya awali,jengo la utawala la walimu,matundu 2 ya choo ya walimu pamoja na kichomea taka.
Makamu Mwenyekiti UWT Taifa Zainab Shomari akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Jitegemee
Makamu Mwenyekiti UWT Taifa akizungumza na wanafunzi Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464