SHINYANGA WAMETOKA NA CLEAN SHEET MIRADI YA MAENDELEO ILIYOMULIKWA NA MWENGE WA UHURU


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kwa ajili ya kuanza kukimbizwa Mkoani humo na kumulika Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Vibe la Mwenge mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikimbiza Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuukabidhi mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akionyesha furaha baada ya kupata Clean Sheet kwenye miradi ya maendeleo iliyomulikwa na Mwenge wa Uhuru.
Vibe likiendelea makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka mkoani Shinyanga kwenda Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiburudika.
Vibe likiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (kushoto) akiwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.

Shinyanga watoka na clean Sheet miradi ya maendeleo Mwenge wa Uhuru

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkoa wa Shinyanga umepongezwa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, ambapo katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani humo miradi yote 41 imepeta hakuna hata mmoja ambao umekataliwa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim, ametoa pongezi hizo leo Agosti 2, 2023 wakati wa Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Shinyanga kwenda Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Abdalla Shaib Kaim.

Amesema Mkoa wa Shinyanga wameupiga Mwingi kwenye Miradi ya Maendeleo, wametoka na Clean Sheet na hakuna mradi hata mmoja ambao wameukataa, huku viongozi wakionyesha ushirikiano wa kutosha.

"Mkuu wa Mkoa Shinyanga umeupiga mwingi umesimamia vyema miradi ya maendeleo umetuheshimisha umeupiga mwingi mmetoka na Cleen Sheet kwenye miradi yote," amesema Kaim.

Aidha, amewasihi viongozi wa Mkoa huo wa Shinyanga waendelee na kasi hiyo hiyo ya kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambayo bado inaendelea kutekelezwa.
Wakuu wa wilaya, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, (katikati)Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, (kulia)ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema kwa upande wa miradi ya maendeleo ambayo imewekewa mawe ya msingi, wataendelea kuisimamia ili itekelezwe kwa kiwango na ubora unaotakiwa.

Amesema Mwenge huo wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Shinyanga, umekimbizwa umbali wa Kilomita 571.5 na kupitia Miradi ya Maendeleo 41 yenye thamani ya Sh.bilioni 14.2.

Aidha, Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Shinyanga ulianza kukimbizwa Julai 27 mwaka huu, na umekabidhiwa leo Agosti 2 mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, (kushoto)akimpatia Cheti cha Pongezi Mkimbiza Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kutoa vyeti vya pongezi kwa wakimbiza Mwenge.
Vyeti vya Pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya Pongezi vikiendelea kutolewa.
Vyeti vya Pongezi vikiendelea kutolewa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464