Mkurugenzi
wa taasisi za shule ya sekondari Anderlek Ridges, shule ya msingi Rocken Hill na Rocken
Hill Academy. Alexander Kazimili akitoa ushauri kwa wazazi juu ya malezi.
Na Kareny Masasy,Kahama
WATOTO wametakiwa kuongoza na wazazi wao katika ulimwengu huu wa kidigital na sio wazazi kuwapa malezi ya kuwadekeza hali ambayo imewakuta watoto wengi nakuwafanya kuharibikiwa katika mstakabali wa maisha yao yote.
Hayo yamesemwa na Naibu makamu mkuu wa chuo cha Mipango,fedha na utawala (TIA) dk Hassanal Issaya alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 15 ya shule ya sekondari Anderlek Ridges na shule ya msingi Rocken Hill na Rocken Hill Academy.
Dk Issaya amesema wazazi wengi wameonekana kuwapenda watoto wao zaidi hadi kuharibikiwa wanatakiwa waelezwe maisha na namna ya kuishi kumbuka watoto wamekuwa na ufahamu mkubwa ukiwapa kuigiza kwa vitendo maisha yalivyo wanaweza kinachotakiwa ni kuwapatia muongozo mzuri wa wenye maisha bora.
“Dunia ya sasa ipo kwenye utandawazi na hautakiwi kutumia mabavu la sivyo dunia itakuacha na wanafunzi wanamaliza watakwenda majumbani na mitaani watakutana na utandawazi kitu cha ushauri wazazi wawe makini katika malezi na simu zitumike kuongeza ujuzi wa elimu sio mambo mengine”alisema dk Issaya.
Dk Issaya amesema katika maisha hakuna kubahatisha na mtu lazima uwe na ndoto kwa kuweka malengo yenye mikakati dhabiti na kuchukua hatua ili kuyafikia malengo hayo yatimie.
“Hivi sasa watoto wengi wanakimbilia mziki zamani tuliona ni uhuni na ukicheza mpira nakurudi jioni mzazi anakuchapa nakulazimishwa upende anachotaka mzazi hivyo muwaache wanachokipenda na kukiendeleza huko nako wanaweza kuwa matajiri.”amesema dk Issaya.
Mkurugenzi wa taasisi za shule hizo Alexander Kazimili akieleza katika mahafali hayo aliwataka wanafunzi yale waliyojifunza shuleni wakayaendeleze huko mitaani waendako kwani wazazi wamewapa zawadi kubwa na bora ya Elimu ambayo ni rasilimali isiyoisha.
“Maisha ni magumu kama una Elimu na Ujuzi ni rasilimali tosha na bahati wanayoitaka ni kuvaa viatu vya kujishughulisha kwa bidii kwani vijana wengi wanataka maisha ya kubahatisha na wakati wote muda uko sahihi na utandawazi uliopo mtaji wake ni akili “alisema Kazimili.
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Anderlek Ridges Godwin Ng’osha amesema wahitimu wa kidato cha nne ni 161 na mkurugenzi wa shule ya msingi Rocken Hill Zephania Madaha amesema wahitimu ni 174 na walieleza wanafunzi wamekuwa wakifundishwa maadili ya kidini na nidhamu katika maisha watakayo yapitia.Naibu makamu mkuu wa chuo cha Mipango,fedha na
utawala (TIA) dk Hassanal Issay mgeni rasmi .
Naibu makamu mkuu wa chuo cha Mipango,fedha na
utawala (TIA) dk Hassanal Issaya