Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari amewataka wanawake kuwalea watoto wao kwa kufuata misingi ya maadili ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuacha kufumbia macho matukio ya ukatili wa kijinsia yanapotokea.
Hayo ameyasema leo Agosti 25/2023 wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Idukilo na Maganzo kwa nyakati tofauti Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ,ambapo amesema maadili yameporomoka katika jamii na kuchangia vitendo vya ukatili kuongezeka ukiwemo ubakaji na kulawiti watoto.
Amesema wanawake ni jeshi kubwa wanapaswa kuwa imara katika kukemea vitendo hivyo ili kuvikomesha kwa kushirikiana na jamii na wadau wengine wa kupinga vitendo hivyo kwa kuunganisha nguvu ya pamoja katika kupaza sauti.
Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti UWT Taifa amewataka wakinamama kuachana na mikopo ambayo inasababisha kuchukuliwa mali zao na wengine kukimbia familia kutokana na mikopo umiza.
Naye Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba amesema kutokana na wakinamama wengi kuumizwa na mikopo umiza serikali imeamuwa kuja na mpango mwingine ambao utawezesha hata mtu binafsi kupata mkopo hatua ambayo itakuwa ni mkombozi kwa wanawake.
Amesema kuendelea kuficha matukio kuna changia matukio hayo kuendelea kutokea na kuathiri watu wengi ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki watoto kuendelea na elimu .
Katika ziara ya viongozi wa UWT
Taifa ambao ni Mwenyekiti Mary Chatanda na Makamu wake Zainab Shomari
imegawanyika katika makundi nane kwa lengo la kuwafikia wananchi Vijijini kwa
haraka katika Kata zote za Wilaya ya Kishapu,ambapo atakuwa na ziara ya siku
nne Mkoani Shinyanga na atatembelea Wilaya zote .
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akizungumza na wakazi wa Maganzo pamoja na Kata jirani Idukilo,Mwaduilohumbo na Songwa kwenye mkutano wa hadhara